Mfalme Amazia
Mandhari

Mfalme Amazia (kwa Kiebrania: אֲמַצְיָהוּ, ʼĂmaṣyāhū, yaani "Nguvu ya YHWH"; 822 KK hivi - 767 KK hivi) alitawala ufalme wa Yuda kati ya miaka 796 KK na 767 KK baada ya baba yake Yehoashi kuuawa.
Alianza kwa kumtumikia YHWH, Mungu pekee wa Israeli, lakini baada ya kushinda Waedomu, alitumikia miungu yao pia, na kwa kiburi alipigana vita na Yehoashi wa Israeli akashindwa vibaya.
Amazia alipouawa, aliyemrithi ni mwanae Uzia.
Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 14 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 25.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mfalme Amazia kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |