Method Kilaini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Method Kilaini (amezaliwa Katoma, Bukoba, 30 Machi 1948) ni askofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania anayehudumia kama askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Askofu Kilaini alipewa upadrisho kama padre wa jimbo la Bukoba jijini Roma mwaka 1972 na Kardinali Agnelo Rossi baada ya kupata shahada ya pili ya teolojia huko Roma.

Baada ya kurudi nyumbani Bukoba, Tanzania, alifanya kazi parokiani, baadaye alikuwa mhazini msaidizi wa jimbo.

Kati ya mwaka 1978 hadi 1985 alifundisha Historia ya Kanisa katika Seminari Kuu ya Ntungamo.

Mwaka 1985 alirudi Roma na kupata shahada ya udaktari wa tauhidi katika Historia ya Kanisa kutoka chuo Kikuu cha Gregoriana mwaka 1990.

Mwaka 1990 hadi 2000 alikuwa Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.

Kuanzia mwaka 2000 alikuwa askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam hadi mwaka 2009 alipoteuliwa kuwa askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Method Kilaini kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.