Meno ya plastiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Meno ya plastiki (kwa Kiingereza: tooth buds) ni jina vinalopewa vijino vinavyoonekana kwenye fizi za mtoto kama uvimbe mweupe wa kung'aa. Meno changa hayo hayajapata madini ya kutosha na huwa laini, ndiyo maana huitwa “meno ya plastiki”.

Dhana potovu[hariri | hariri chanzo]

Katika Ulimwengu wa Tatu, Afrika Mashariki ikiwemo, meno hayo yanawapa wasiwasi wazazi wengi kutokana na dhana potovu ya kwamba ni minyoo ndani ya meno na kwamba yanaleta madhara kama vile kutapika, kuharisha na kupatwa na homa kwa mtoto.

Dhana hiyo husababisha watoto wengi wenye umri wa miezi 6 hadi 24 kutolewa meno hayo kana kwamba kuyatoa ndiyo suluhisho pekee la mtoto kupona.

Vijijini Kenya katika kundi la watoto 95 wenye umri kati ya miezi sita na miaka miwili waliotahiniwa mwaka 1991/92, 87% walipatikana kuwa wameng'olewa jino moja au zaidi. Katika kundi la watoto wa umri wa miaka 3-7, 72% ya watoto walikuwa hawana magego. [1][2] [3]

Utafiti unaonyesha kuwa waganga wa jadi ndio wanaosambaza habari hizo na kuleta hofu kwa wazazi kwamba meno hayo yasipotolewa huweza kusababisha kifo cha mtoto.

Maelezo ya kisayansi[hariri | hariri chanzo]

Mtoto anapofikia umri wa kouta meno, fizi huvimba na mara nyingi vijitoto vya meno huonekana ndani ya fizi katika maeneo ambayo meno hutokea baadae. Vijino hivyo havina uhusiano wowote na mtoto kuumwa bali viko pale kama ishara ya meno yatakayoota mdomoni.

Elimu kubwa inahitajika kwa jamii ili kuondoa imani potovu na kutunza afya ya kinywa na meno ya watoto. Tujifunze kila siku kuhusu mambo yanayojadiliwa mitaani ili kujua ukweli na kupeleka elimu sahihi kwa jamii.

Madhara ya kutoa meno hayo[hariri | hariri chanzo]

Madhara ya kutoa meno hayo ni kama ifuatavyo:

  1. maumivu makali kwa mtoto kwani waganga hao hawatumii ganzi
  2. magonjwa ya kuambukiza kama HIV na homa ya ini maana vifaa vinavyotumika huwa si salama
  3. vijino hivyo vikitolewa vyote mtoto atakosa kabisa meno hayo mdomoni na vikitolewa nusu tu jino bovu huota hapo baadaye
  4. katika kutoa vijino hivyo meno ya pembeni yanaweza kudhurika na hata kuota vibaya hapo baadaye.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Hassanali J, Amwayi P, Muriithi A (Apr 1995). "Removal of deciduous canine tooth buds in Kenyan rural Maasai". East Afr Med J 72 (4): 207–9. PMID 7621751. 
  2. Hiza JF, Kikwilu EN (Apr 1992). "Missing primary teeth due to tooth bud extraction in a remote village in Tanzania". Int J Paediatr Dent 2 (1): 31–4. PMID 1525129. 
  3. "mchoro". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-23. Iliwekwa mnamo 2020-06-23. 
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Meno ya plastiki kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.