Nenda kwa yaliyomo

Meli ya starehe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Meli za starehe)
Meli ya starehe ya Marekani.
Meli ya starehe huko Marekani.
Meli ya starehe katika mfereji wa Panama.
Meli "Harmony of the Seas".
Meli "Disney Fantasy".

Meli ya starehe (kwa Kiingereza: Cruise) ni chombo cha usafiri kiendacho majini ambacho hutumika si kusafirisha mizigo mizito kama vile magari na vitu vingine vingi, lakini hata kusafiriha watu kwa lengo la starehe, si lingine. Meli hizo huwa kubwa sana, zenye fahari nyingi ndani yake kama vile sehemu za kuogelea, sehemu za michezo, miziki, chakula, vinywaji na mambo mengineyo. Safari zake huwa za muda mrefu kwa sababu huendeshwa kwa mwendo wa kawaida, hivyo huchukua siku tatu na zaidi kulingana na umbali wa sehemu zinakoelekea.

Usafiri huo huwa mzuri na wenye usalama ijapokuwa unaweza kusumbuliwa na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo huweza kusababisha mawimbi makali baharini au ziwani, hivyo mara nyingi kabla vyombo hivi havijaanza safari hufanyiwa marekebisho, na manahodha huwa na mawasiliano na mamlaka ya hali ya hewa nchini humo ili kuweza kuchukua tahadhari.

Mbali na Marekani meli hizi hupatikana sehemu mbalimbali za ulimwengu kama vile Dubai, Italia, Brazil, Argentina n.k. Meli hizi zina uwezo wa kuchukua idadi ya abiria mpaka 8,000 kwa wakai wa sasa na zinasaidia sana kukuza utalii duniani.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Meli ya starehe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.