Nenda kwa yaliyomo

Meli za abiria Marekani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Meli ya abiria ya Marekani.
Meli ya abiria huko Marekani.
Meli katika mfereji wa Panama.
Meli "Harmony of the Seas".
Meli "Disney Fantasy".

Meli ni chombo cha usafiri kiendacho majini. Chombo hicho hutumika hasa katika kusafirisha mizigo mizito kama vile magari na vitu vingine vingi, lakini hata kusafiriha watu.

Kwa mfano nchini Marekani meli hutumika kubebea mizigo pia hutumiwa na watu katika safari nchini humo. Meli hizo hujulikana kwa jina la Cruise. Meli hizi huwa kubwa sana, zenye fahari nyingi ndani yake kama vile sehemu za kuogelea, sehemu za michezo,miziki, kula na kulala.

Safari zake huwa za muda mrefu kwa sababu huendeshwa kwa mwendo wa kawaida, hivyo safari zake huchukua takriban siku tatu na zaidi kulingana na umbali wa sehemu zinakoelekea. Mbali na hili ni kwa sababu meli hizi huwa na mahitaji ya kutosha kwa ajili ya kila mtu, kama vile chakula, vinywaji na mambo mengineyo kama vile michezo.

Usafiri huu huwa mzuri na wenye usalama ijapokuwa unaweza kusumbuliwa na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo huweza kusababisha mawimbi makali baharini au ziwani, hivyo mara nyingi kabla vyombo hivi havijaanza safari hufanyiwa marekebisho, na manahodha huwa na mawasiliano na mamlaka ya hali ya hewa nchini humo ili kuweza kuchukua tahadhari.

Mbali na Marekani meli hizi hupatikana sehemu mbalimbali za ulimwengu kama vile Dubai, Italia, Brazil, Argentina n.k. Meli hizi zina uwezo wa kuchukua idadi ya abiria mpaka 8,000 kwa wakai wa sasa na zinasaidia sana kukuza utalii duniani.