Nenda kwa yaliyomo

Mbwana Samatta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mbwana Samatta
noborder
Maelezo binafsi
Jina kamiliMbwana Aly Samatta
tarehe ya kuzaliwa23 Desemba 1992 (1992-12-23) (umri 33)
mahali pa kuzaliwaDar es Salaam, Tanzania
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasaLe Havre
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2010–2011Simba25(13)
2011–2016TP Mazembe103(60)
2016–2020Genk144(56)
2020– 2020Aston Villa14(1)
2020 - 2023Fernabahce30(5)
2021 - 2022Antwerp (mkopo)32(5)
2021 - 2022Genk (mkopo)33(6)
2023 - 2025PAOK41(6)
2025 -Le Havre0(0)
Timu ya Taifa ya Kandanda
Tanzania83(22)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only.

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 15 September 2024

Mbwana Ally Samatta, (alizaliwa 23 Disemba 1992), ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Tanzania katika klabu ya Feberbahce nchini Uturuki [1]. Mbwana ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na kabla ya kuhamia klabu ya Feberbahce (Uturuki) alikuwa akucheze timu ya Aston Villa nchini Uingereza[2].

Samatta alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya African Lyon F.C. mwaka 2008 nchini Tanzania. Alisajiliwa na klabu ya Simba mwaka 2010, ambapo alicheza katika nusu msimu tu kabla ya kujiunga na klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Alicheza kwa miaka mitano ndani ya TP Mazembe na kujijengea nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Mwaka 2015, alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka wa Afrika, na kumaliza msimu akiwa mfungaji bora wa mashindano ya klabu bingwa Afrika (Ligi ya Mabingwa Afrika) na kuisaidia klabu yake kushinda taji hilo.

Samatta alijiunga na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji mnamo januari 2016, aliisaidia kufuzu michuano ya Ulaya maarufu kama Europa Ligi na kushinda taji la ligi ya Ubelgiji (Belgian Jupiler Ligi mwaka 2019. Alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo akashinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe award)[3].

Manamo Januari mwaka 2020, Samatta alisajiliwa na klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza na kuwa mchezaji wa kwanza kutoka nchini Tanzania kucheza na kufunga goli ligi kuu ya nchini Uingereza.

Samatta alikua mchezaji muhimu wa TP Mazembe waliposhinda taji la klabu bingwa Afrika mwaka 2015 (2015 CAF Champions Ligi), akifunga jumla ya magoli saba na kumaliza akiwa mfungaji bora.[4]

Mnamo Januari 2016, aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea Afrika ya Mashariki kutwaa tuzo hiyo. Katika ugawaji wa tuzo hizo uliofanyika jijini Abuja, Nigeria, tarehe 7 Januari 2016, Samatta alikusanya jumla ya alama 127, akimzidi mchezaji mwenzake Robert Kidiaba mlinda lango wa TP Mazembe na timu ya taifa ya DR Congo aliyepata alama 88. Baghdad Bounedjah raia wa Algeria alishika nafasi ya tatu akiwa na alama 63.[5] Katika mchezo dhidi ya Moghreb Tétouan ya Moroko, Samatta alifunga magoli matatu kwa mpigo (hat-trick) yaliyowafanya wasonge hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika. Magoli hayo yanakumbukwa sana katika historia ya klabu ya TP Mazembe.[6]

Muda mfupi baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, alijiunga na klabu ya K.R.C. Genk kwa mkataba wa miaka minne na nusu.[7] Tarehe 23 Agosti 2018 Samatta alifunga goli tatu kwa mpigo(hat-trick) dhidi ya Brøndby IFkwenye mashindano ya Ulaya maarufu kwa jina la Europa Ligi walfanikiwa kupata ushindi wa goli 5–2.[8] Mei 2019 aliishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe).

Aston Villa

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Januari 20, 2020, Samatta alijiunga na klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi Kuu ya Uingereza kwa mkataba wa miaka minne na nusu.[9] Uhamisho huu ulimfanya Samatta kuwa mchezaji wa kwanza wa kitanzania kucheza ligi kuu ya Uingereza.[10] Ada ya uhamisho inakadiriwa kuwa £8.5 milioni.[11][12] Mchezo wa kwanza alicheza siku nane baada ya kusajiliwa dhidi ya Leceister City kwenye mzunguku wa pili wa mashindano ya Carabao hatua ya nusu fainali, waliibuka na ushindi wa magoli 2 – 1, kwa matoke ohayo, Villa walifika hatua ya fainali.[13]

Samatta alifunga goli lake la kwanza manamo 1 Februari 2020, walipocheza na Bournemouth, mchezo ulimalizika kwa Villa kushinda magoli 2 - 1. Goli hilo lilimfanya Samatta kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza na kufunga kwenye mashindano ya Ligi ya Uingereza.[14]

Fenerbahçe

[hariri | hariri chanzo]

Samatta alijiunga na Klabu ya Fernabahce ya nchini Uturuki tarehe 25 Septemba 2020, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.[15] Ulipofika mwisho wa mkopo mnamo Julai 2021, Samatta alisaini mkataba wa miaka minne, hii ilikua ni sehemu ya makubaliano ya uhamisho wake.[16]

Tarehe 1 Septemba 2021, Samatta alijiunga na Royal Antwerp ya nchini Ubelgiji kwa mkopo wa msimu mzima.[17]

Ilipofika 16 Agosti 2022, Samatta alirudi tena Genk kwa mkopo, uhamisho huo ulikua na chaguo la Genk kumnunua.[18]

Mnamo tarehe 17 Julai 2023, timu ya nchini Ugiriki PAOK ilitangaza kumsajili Samatta kwa mkataba wa miaka miwili, mkataba huo ulikua na nafasi ya kuongeza mwaka mmoja.[19]

Le Havre

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Agosti 5 2025, Klabu inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa Le Havre ilitangaza kumsajili Samatta bila ya gharama ya usajili. Usajili huo ulimfanya Samatta kuwa mchezaji wa kwanza wa Kitanzania kucheza ligi hiyo.[20]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Mbwana Samatta ni Mndengereko kutoka Kibiti kwa kabila. Katika maisha ya imani ni Muislamu.[21]

Takwimu za michezo

[hariri | hariri chanzo]
Michezo na magoli ya klabu, Msimu na mashindano
KlabuMsimuLigiCupKombe la ligiYa BaraMengineyoJumlaRef.
UshindaniMichezoMagoliMichezoMagoliMichezoMagoliMichezoMagoliMichezoMagoliMichezoMagoli
Simba S.C.2010–11Ligi Kuu Tanzania Bara 2513[tanbihi 1]22515 [22][23]
TP Mazembe2011Linafoot 8282 [22][23]
2012 2923963729 [22][23]
2013 3720554225 [22][23]
2013–14 2915843719 [22][23]
2014–15 6464 [23]
2015–16 6464 [23]
Jumla 103600033230013683
K.R.C. GenkLigi kuu ya Ubelgiji 620012[tanbihi 2]3185 [24]
2016–17 27104218510[tanbihi 2]35920 [24]
2017–18 2044011[tanbihi 2]4358 [24]
2018–19 28201012910[tanbihi 2]35132 [24]
Jumla 813692003014431316365
Jumla maisha ya soka 209109920063394313324163

Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

[22]

Taifa Stars
MwakaMichezoMagoli
201192
201240
2013106
201431
201572
201641
201733
201852
201961
Total5118

Magoli Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]
GoliTareheUwanjaMpinzaniAlamaMatokeoMashindano
1.26 Machi 2011Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Tanzania Jamhuri ya Afrika ya Kati2–12–1kufuzu AFCON 2012
2.3 Septemba 2011 Aljeria1–01–1
3.11 Januari 2013Uwanja wa Adis ababa, Addis Ababa, Ethiopia Ethiopia1–11–2Mchezo wa Kirafiki
4.6 Februari 2013Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Kamerun1–01–0
5.24 Machi 2013 Moroko2–03–1kufuzu fainali za kombe la dunia 2014
6.3–0
7.4 Disemba 2013Uwanja wa Afraha, Nakuru, Kenya Burundi1–01–0hatua ya makundi mashindano ya CECAFA 2013
8.12 Disemba 2013uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya Zambia1–11–1mashindano ya CECAFA hatua ya mtoano 2013
9.3 Agosti 2014uwanja wa Estádio do Zimpeto, Maputo, Msumbiji Msumbiji1–11–2Kufuzu AFCON 2015
10.7 Oktoba 2015Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania Malawi1–02–0kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 hatua ya kwanza
11.14 Novemba 2015 Aljeria2–02–2kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 – hatua ya pili
12.23 Machi 2016uwanja wa Stade Omnisports Idriss Mahamat Ouya, N'Djamena, Chad Chad1–01–0kufuzu AFCON 2017 hatua ya makundi
13.25 Machi 2017Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania Botswana1–02–0Mchezo wa kirafiki
14.2–0
15.10 Juni 2017 Lesotho1–01–1kufuzu AFCON 2019 Kundi L
16.27 Machi 2018 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo1–02–0Mchezo wa kirafiki
17. 16 Oktoba 2018  Cabo Verde2–02–0kufuzu AFCON 2019
18.27 Juni 2019uwanja wa 30 June Stadium, Cairo, Misri Kenya2–12–3AFCON 2019 Kundi C
19.8 Septemba 2019Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania Burundi1–01–1 (3–0 mikwaju ya penalti)kufuzu michano ya kombe la dunia 2022 hatua ya kwanza

TP Mazembe[25]

  • Linafoot: 2011, 2012, 2013, 2013–14
  • DR Congo Super Cup: 2013, 2014
  • Klabu bingwa Afrika: Klabu bingwa Afrka 2015[26][27]

Genk

  • Ligi kuu ya Ubelgiji: msimu wa 2018–19[28]
  • Belgian Super Cup: michuano ya pili ya Ubelgiji 2019[29]

Binafsi

  • Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika: 2015
  • Timu yam waka ya CAF: 2015[30]
  • Mfungaji bora ligi ya mabingwa Afrika: 2015[4]
  • Mchezaji bora ligi ya Ubelgiji: 2019[3]
  • Mfungaji bora ligi ya Ubelgiji: msimu wa 2018-19[29]
  1. "Mbwana Samatta Fenerbahçemizde". Fenerbahce Official Site. 25 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link)
  2. https://www.thecitizen.co.tz/news/Sports/Mbwana-Samatta-joins-Fenerbahce-on-loan/1840572-5627064-au6qg8/index.html
  3. 1 2 Barrie, Mohamed Fajah (7 Mei 2019). "Tanzania's Mbwana Samatta wins Belgium's Ebony Shoe award". BBC Sport. Iliwekwa mnamo 28 Agosti 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 1 2 "TP Mazembe beat USM Alger to win African Champions Ligi". BBC Sport. 8 Novemba 2015. Iliwekwa mnamo 25 Agosti 2016.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Tanzania's Samatta is African Player of the Year Based in Africa". www.kawowo.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-01-27. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Gondwe, Kennedy (20 Septemba 2015). "Mazembe's Tanzania star Samatta harbours European hopes". BBC Sport. Iliwekwa mnamo 7 Januari 2018.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Mbwana Samatta signs for Belgian side Genk". BBC Sport. 29 Januari 2016. Iliwekwa mnamo 25 Agosti 2016.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Tosin Morakinyo (23 Agosti 2018). "Mbwana Samatta's hat-trick fires Genk past Broendby IF". Goal.com. Iliwekwa mnamo 4 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Styles, Greg (20 Januari 2020). "Samatta signs for Aston Villa". Aston Villa Football Club. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 21 Januari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Kwenda, Stanley (3 Februari 2020). "Mbawana Samatta thrilled to be Tanzanian trailblazer". BBC Sport. Iliwekwa mnamo 11 Januari 2024.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Mbwana Samatta: Aston Villa sign Genk's Tanzania striker for £8.5m". BBC Sport. 20 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 21 Januari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Aston Villa confirm signing of Mbwana Samatta". Express and Star. 20 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 31 Januari 2020.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. "Aston Villa 2-1 Leicester (3-2 agg): Wembley for Villa after Trezeguet goal in stoppage-time". Sky Sports. 28 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 29 Januari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. Oludare, Shina (1 Februari 2020). "Aston Villa's Samatta sets four records on Premier League debut". Goal.com.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "Villa's Samatta joins Fenerbahce on loan". BBC Sport.
  16. Chuma, Festus (3 Julai 2021). "Mbwana Samatta Becomes Permanent Fenerbahce Player". Ducor Sports. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-07-03. Iliwekwa mnamo 2024-10-16.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  17. Oludare, Shina (1 Septemba 2021). "Mbwana Samatta: Royal Antwerp sign Fenerbahce striker | Goal.com". www.goal.com. Iliwekwa mnamo 3 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  18. "Welkom terug Ally Samatta". KRC Genk (kwa Kiholanzi). 16 Agosti 2022. Iliwekwa mnamo 17 Agosti 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  19. "Παίκτης του ΠΑΟΚ ο Άλι Σαμάτα" (kwa Kigiriki). PAOK FC. 17 Julai 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-04-20. Iliwekwa mnamo 17 Julai 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  20. "Samatta becomes first Tanzanian to join French Ligue 1, joins Le Havre on one-year deal" (kwa Kigiriki). The Citizen. 5 Agosti 2025. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  21. Kaorata, Salum (30 Mei 2018). "Picha: Mbwana Samatta atua Mecca kufanya Umrah". Bongo5.com (kwa Swahili). Iliwekwa mnamo 28 Septemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
  22. 1 2 3 4 5 6 "Mbwana Aly Samata". National Football Teams. Iliwekwa mnamo 5 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  23. 1 2 3 4 5 6 7 Mbwana Samatta at Soccerway. Retrieved 4 April 2018.Kosa la hati: Hakuna moduli kama "EditAtWikidata".
  24. 1 2 3 4 "Mbwana Samatta » Club matches". worldfootball.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-04. Iliwekwa mnamo 20 Oktoba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  25. "Mbwana Samatta is carrying Tanzania's torch in Europe". First Touch. 3 Machi 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-12. Iliwekwa mnamo 12 Julai 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  26. "Advantage Mazembe in CAF final after away win". CAF. 1 Novemba 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  27. "Mazembe beat USMA to reach fifth heaven". CAF. 8 Novemba 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  28. "Tanzania captain Mbwana Samatta linked with move to Middlesbrough". Goal. 3 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 12 Julai 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  29. 1 2 "Landskampioen Genk opent seizoen met Supercup-winst tegen KV Mechelen". Sporza. 20 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 21 Julai 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  30. "Aubameyang, Samatta Rule Africa". CAF. Januari 7, 2016. Iliwekwa mnamo Januari 7, 2016.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  1. Inakosa idadi ya michezo
  2. 1 2 3 4 Includes Belgian First Division A playoffs