Nenda kwa yaliyomo

Mbwa wa polisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mbwa wa polisi (jina halisi ni German Shepherd) pia anajulikana huko Uingereza kama Alsatian, ni mbwa wa kazi wa kuzalishwa kutoka nchini Ujerumani. Mbwa huyu ana ukubwa wa kati hadi ukubwa zaidi. Kizazi hiki kilianzishwa na Max von Stephanitz mwaka wa 1899 kwa kutumia aina mbalimbali za mbwa wa kale wa malisho wa Kijerumani.

Kiasili, mbwa huyu alizalishwa kwa ajili ya kuchunga kondoo. Baadaye, alitumika kwa kazi nyingine nyingi kama vile mbwa msaidizi wa walemavu, mbwa wa uokoaji, mbwa wa polisi, na hata katika vita. Leo hii, anafugwa sana kama mbwa wa kufugwa majumbani. Kulingana na Fédération Cynologique Internationale, alikuwa wa pili kwa usajili wa kila mwaka mwaka 2013.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Max von Stephanitz, mwanzilishi wa kizazi hiki (akiwa na Horand von Grafrath), karibu mwaka 1900
Mchoro kutoka mwaka 1909

Katika miaka ya 1890, kulikuwa na jitihada za kuweka viwango vya kisayansi vya aina za mbwa.[1] Mbwa walikuwa wakizalishwa kwa lengo la kudumisha sifa zilizosaidia kazi ya kuchunga kondoo na kuwalinda dhidi ya wanyama hatari. Hili lilifanyika katika jamii za vijijini nchini Ujerumani, ambapo wachungaji walichagua mbwa bora wa kuzalisha. Walitambua kuwa mbwa hawa walikuwa na sifa muhimu kama vile akili, kasi, nguvu, na uwezo mkubwa wa kunusa. Hata hivyo, mbwa walikuwa tofauti sana kati ya maeneo mbalimbali, kwa sura na uwezo. [1]

Ili kuondoa tofauti hizi, klabu ya mbwa ya Phylax Society iliundwa mwaka 1891 kwa lengo la kuunda mpango wa viwango vya uzalishaji wa mbwa wa kienyeji nchini Ujerumani. Lakini ilivunjika baada ya miaka mitatu kutokana na tofauti za maoni kuhusu kama mbwa wazalishwe kwa minajili ya kazi au muonekano. Ingawa haikufanikiwa, asasi hiyo iliwatia moyo watu wengine kuendeleza jitihada hizo wao binafsi.

Wakati miji mikubwa ya viwanda ikikua nchini Ujerumani, idadi ya wanyama wanaowinda ilipungua, hivyo kufanya kazi ya mbwa wachungaji kupoteza umuhimu. Lakini watu walianza kuona mbwa wa kuchunga kama viumbe werevu na wenye uwezo mkubwa. Max von Stephanitz, aliyekuwa afisa wa farasi na mwanafunzi wa zamani wa Chuo cha Mifugo cha Berlin, aliamini kuwa mbwa wa kazi walipaswa kuzalishwa kwa ajili ya kazi maalumu,

Mwaka 1899, alihudhuria maonyesho ya mbwa ambapo alikutana na mbwa aitwaye Hektor Linksrhein. Hektor alikuja na matokeo ya kizazi cha mbwa waliopandwa kwa makusudi maalum. Tena wa mfano bora kwa kile von Stephanitz alichotamani kitokee. Akamnunua upesi, akambadilishia jina kuwa Horand von Grafrath, na kuanzisha Verein für Deutsche Schäferhunde (Jumuiya ya Mbwa Wa Kijerumani).[1] Horand alikuwa mbwa wa kwanza kusajiliwa kama German Shepherd. Kufikia 1923, jumuiya hiyo ilikuwa na wanachama 50,000 nchini Ujerumani pekee.[2]

Horand alitumika sana katika uzalishaji wa kizazi kipya na alizaliana na mbwa wengine waliokuwa na sifa zinazotakiwa. Kupitia mchakato wa uzalishaji wa karibu (inbreeding), uzao wa Horand uliweza kudhibiti sifa bora. Mbwa wote wa kizazi cha German Shepherd leo wanahusiana na uzao huu wa awali.

Katika nusu ya kwanza ya karne ya ishirini, mbwa huyu aliunganishwa sana na Ujerumani ya kifalme na ya Kinazi kutokana na wazo la usafi wa nasaba na utimilifu wa kijeshi. Adolf Hitler alipenda sana mbwa hawa na alikuwa na mbwa kadhaa wa aina hii, akiwemo Blondi, aliyekufa kwa jaribio la sumu ya cyanide katika Führerbunker kabla ya Hitler kujiua. Pia walitumiwa kama walinzi katika kambi za mateso za Kinazi.[3]

Sable jike (kushoto) na dume (kulia)

Kizazi hiki kilitajwa na von Stephanitz kama Deutscher Schäferhund, ikimaanisha "Mbwa wa Mchungaji wa Kijerumani".Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; refs with no name must have content Jina hilo lilitumiwa rasmi kwenye kitabu cha vizazi. Baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, neno "Kijerumani" lilionekana kuwa na athari mbaya kwenye umaarufu wa mbwa hawa, hasa katika nchi zilizopigana na Ujerumani.

Kwa hiyo, Klabu ya Mbwa ya Uingereza waliwaita jina la "Alsatian Wolf Dog", wakitumia jina la eneo la Alsace lililoko mpakani mwa Ufaransa na Ujerumani. Hatimaye, neno "Wolf Dog" liliondolewa, lakini jina la "Alsatian" lilibaki hadi 1977, ambapo wapenda mbwa walifanikiwa kurudisha jina la "German Shepherd" nchini Uingereza.Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; refs with no name must have content

Mifupa kwenye Jumba la Mifupa ya Mifugo FMVZ USP São Paulo, Brazil

German Shepherd ni mbwa wa kati hadi mkubwa zaidi.[4] Kiwango cha urefu kwa dume ni cm 60–65 (in 24–26), na kwa jike ni cm 55–60 (in 22–24).

Wanauwezo wa kukimbia haraka hadi miles per hour 30 (km/h 48).[5] Miili yao ni mirefu kuliko kimo chao wakisimama, na vichwa vyao vina paji la uso lenye umbo la duara, midomo mirefu ya mraba, pua nyeusi, macho ya rangi ya kahawia, na masikio makubwa yaliyosimama.

German Shepherd wana manyoya mawili: koti la nje na koti la ndani. Kuna aina mbili za manyoya: ya kati na marefu. Aina ya manyoya marefu ni nadra zaidi kwa sababu ni ya kurithiwa kwa njia ya jini linalojificha.

  1. 1.0 1.1 1.2 "History of the breed". German Shepherds.com. 30 Desemba 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Juni 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Skabelund, Aaron (Juni 2008). "Breeding racism: The imperial battlefields of the 'German' shepherd dog" (PDF). Society and Animals. 16 (4): 355. doi:10.1163/156853008X357676. ISSN 1063-1119 – kutoka AnimalsAndSociety.org.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Jacobs, Benjamin (18 Januari 2001). The Dentist of Auschwitz: A memoir. University Press of Kentucky. uk. 123. ISBN 0813190126.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Can the German Shepherd Be Saved?". ABC News. 28 Oktoba 2011. Iliwekwa mnamo 21 Agosti 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Purgason, Jason (31 Januari 2021). "15 Of The Fastest Dog Breeds In The World". Highland Canine Training.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)