Nenda kwa yaliyomo

Mbong Amata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mbong Amata (alizaliwa 21 Septemba 1985, jina lake la kuzaliwa ni Odungide) ni mwigizaji kutoka Nigeria. Ameonekana katika filamu kama vile Black November, Forgetting June, na Inale. Alishinda taji la "Msichana Mrembo Zaidi" (Akwa Ibom) mwaka 2003 na alikuwa mshindi wa pili wa pili katika shindano la Miss Nigeria mwaka 2004[1].

Mwaka 2001, katika usaili huko Calabar, alikutana na Jeta Amata. Miaka miwili baadae alipokuwa na miaka 18, walianza kuchumbiana. Walifunga ndoa mwaka 2008 na binti yao Veno alizaliwa baadae mwaka huo huo. Mwaka 2013, walitengana na mwaka 2014 walitalikiana[2].

Amata anaishi kati ya Los Angeles na Lagos. Watu walidhani alikuwa ametoweka, lakini baadae alijitokeza kukanusha habari hiyo kwenye mitandao ya kijamii[3].

  1. ↑ Temitope (2020-09-21). "Mbong Amata clocks 35 today". Vanguard Allure (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-09-28.
  2. ↑ "Marriage not my priority for now –Mbong Amata", The Punch - Nigeria's Most Widely Read Newspaper (kwa American English), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-04-02, iliwekwa mnamo 2026-09-28
  3. ↑ "Mbong Amata". IMDb. Iliwekwa mnamo 2026-09-28.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbong Amata kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.