Mbawavijiko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mbawavijiko
Nemoptera bipennis
Nemoptera bipennis
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Neuroptera (Wadudu walio na mabawa wenye vena nyingi kama kimia)
Nusuoda: Myrmeleontiformia (Wadudu kama vitukutuku)
Familia: Nemopteridae (Wadudu walio na mnasaba na vitukutuku)
Burmeister, 1839
Ngazi za chini

Nusufamilia 2, jenasi 5:

Mbawavijiko ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa familia Nemopteridae katika familia ya juu Myrmeleontoidea wa oda Neuroptera walio na mabawa marefu na membamba ya nyuma. Mabawa hayo ya mbawavijiko wa kweli ni pana zaidi mwishoni na yanafanana na vijiko vyenye mashikio marefu. Spishi za nusufamilia Crocinae huitwa mbawanyuzi, kwa sababu mabawa ya nyuma hayana sehemu pana. Familia hii ina spishi chini ya 200, ambazo hutokea kanda za kitropiki na kinusutropiki duniani kote, isipokuwa Amerika ya Kaskazini, katika maeneno makavu hasa.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida wapevu ni wadudu wakubwa kiasi wenye mabawa ya upana wa mm 25-100. Mabawa ya mbele kwa ujumla ni mapana zaidi kuliko yale ya vitukutuku na mara nyingi yanatoa rangi kama upindemvua. Mabawa ya nyuma ni membamba sana. Katika nusufamilia [[Nemopterinae] hayo yana sehemu pana mwishoni. Walakini, yale ya Crocinae ni membamba katika urefu wao wote. Mbawavijiko na mbawanyuzi wote wana vichwa vidogo vilivyo na macho makubwa kiasi na sehemu za mdomo zinazofanana na pua.

Wadudu hao huruka vibaya kama wapevu wa vitukutuku. Wengi hukiakia usiku, ingawa baadhi ya spishi hukiakia mchana. Hula mbochi na chavua kwa midomo yao mirefu.

Lava wanafanana na vitukutuku, lakini hawachimbi marima. Badala yake, hujificha kwenye mchanga au chini ya takataka na kunyakua wadudu wengine wanaokuja karibu. Wamerefuka zaidi kuliko vitukutuku, hasa spishi za Crocinae, ambazo zina pronoto ndefu hadi ndefu sana.

Spishi za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

  • Dielocroce berlandi (Kenya)
  • Dielocroce chobauti (Kenya)
  • Nemeura glauningi (Kenya, Tanzania)
  • Nemopistha imperatrix (Kenya, Tanzania, Uganda)
  • Nemopistha remipennis (Tanzania)

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]