Maya Horgan Famodu
Maya Horgan Famodu ni mjasiriamali raia wa nchini Nigeria na Marekani, mwanzilishi na mshirika katika Ingressive, kampuni inayotoa huduma kwa makampuni na biashara zinazotanuka kuelekea Afrika.
Pia alianzisha Ingressive Capital, mfuko wa uwekezaji (venture capital) unaowekeza katika makampuni ya teknolojia yaliyopo barani Afrika.[1][2]
Maya ni mmoja wa waanzilishi wa High Growth Africa Summit, mkutano unaohusu kuanzisha biashara zenye mafanikio barani Afrika, na alianzisha Tech Meets Entertainment Summit, kwa ajili ya watu maarufu wa Afrika na makampuni ya teknolojia kujenga ushirikiano wa kuzalisha mapato.[3][4]
Maya pamoja na wenzake, Sean Burrowes na Blessing Abeng, baadaye walianzisha Ingressive for Good, shirika lisilo la kifaida linalotoa ufadhili wa masomo, mafunzo ya kiufundi, na utafutaji wa ajira kwa vijana wa Afrika..[5][6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Onyinye, Yvonne (9 Oktoba 2018). "Maya Horgan Famodu: On Self-Care And Courage". The Guardian. Iliwekwa mnamo 24 Aprili 2019.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Udodiong, Inemesit (27 Machi 2019). "Meet the 10 inspiring women ruling Nigeria's tech ecosystem". Pulse. Business Insider. Iliwekwa mnamo 24 Aprili 2019.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Maya Horgan Famodu: Executive Profile & Biography - Bloomberg". www.bloomberg.com. Iliwekwa mnamo 2019-04-25.
- ↑ Bella Naija (12 Septemba 2018). "Venture Investor Maya Horgan Famodu of Ingressive is our #BellaNaijaWCW this Week". bellanaija.com. Iliwekwa mnamo 24 Aprili 2019.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "How to Start a VC: Interview with Maya Horgan Famodu, Founder, Ingressive Capital". Forbes.
- ↑ "Over 60,000 young Africans trained in Tech by Ingressive for Good, a year after launching". 13 Septemba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maya Horgan Famodu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |