Mavis Chirandu
| Mavis Chirandu | ||
| Maelezo binafsi | ||
|---|---|---|
| Tarehe ya kuzaliwa | 15 Januari 1995 | |
| Mahala pa kuzaliwa | Harare, Zimbabwe, | |
| Maelezo ya klabu | ||
| Klabu ya sasa | Weerams FC | |
| Timu ya taifa | ||
| Zimbabwe | ||
|
* Magoli alioshinda | ||
Mavis Chirandu (amezaliwa 15 Januari 1995) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Zimbabwe anayehudumu katika nafasi ya kiungo. Ameichezea klabu ya Weerams F.C. pamoja na timu ya taifa ya wanawake ya Zimbabwe.[1]
Wasifu na kazi
[hariri | hariri chanzo]Akiwa mtoto mchanga, Chirandu alitelekezwa na mama yake kwenye vichaka kando ya barabara. Alilelewa kwenye kituo cha watoto yatima cha SOS Children's Villages mjini Bindura. Mnamo 2013, aliichezea kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya wanawake ya Zimbabwe katika mchezo dhidi ya Uruguay. Pia , alipata jina la utani "Madam Chair" kutokana na mwenyekiti wa chama cha soka la wanawake la Zimbabwe, Mavis Gumbo. Mnamo mwezi November 2013, Chirandu alifunga bao lake la kwanza katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Lesotho.[2]
Akiwa na umri wa miaka 21, alicheza kama kiungo mkabaji wa kushoto na kujuhishwa katika kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki ya Majira ya Joto 2016.[3] Alifunga bao pekee la kufutia machozi katika dakika za mwisho wa mchezo wao wa hatua ya makundi waliopoteza kwa mabao 3–1 dhidi ya Canada katika Uwanja wa Arena Corinthians, São Paulo.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Muchinjo, Enock (4 Agosti 2016). "Rio 2016: Zimbabwe women's arduous journey to Brazil". Al Jazeera. Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2016.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Mhara, Henry (7 Novemba 2013). "'Madam Chair' scores first Mighty Warriors goal". The Southern Eye (Zimbabwe). Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2016.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Dube, Ngqwele (17 Julai 2016). "Dream come true for baby-dumped Chirandu". The Sunday News (Zimbabwe). Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2016.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Zimbabwe duo savouring Olympic adventure". FIFA. 7 Agosti 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 8, 2016. Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2016.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mavis Chirandu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |