Maurice Piat
Mandhari
Maurice Piat, C.S.Sp. GCSK (alizaliwa 19 Julai 1941) ni kiongozi wa Kanisa Katoliki wa Mauritius ambaye alihudumu kama Askofu wa Port Louis, Mauritius, kuanzia 1993 hadi 2023. Ni mtawa aliyeweka nadhiri katika Shirika la Roho Mtakatifu (Congregation of the Holy Spirit).
Piat alipewa upadirisho mwaka 1970 na kuteuliwa kuwa askofu mwaka 1991. Papa Fransisko alimteua kuwa kardinali tarehe 19 Novemba 2016.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The new cardinals". Vatican News Services. 9 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 14 Oktoba 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |