Mateusz Klich

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mateusz Klich

Mateusz Andrzej Klich (alizaliwa 13 Juni 1990) ni mchezaji wa soka ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya Leeds United na timu ya taifa ya Poland.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Cracovia[hariri | hariri chanzo]

Klich alisajiliwa katika klabu hiyo mnamo Novemba 2008. Wakati wa msimu wa 2009/10, polepole alikua akicheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha watu kumi na moja katika klabu ya Cracovia na baadaye akahamia klabu ya Wolfsburg mwaka 2011.

Wolfsburg[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 14 Juni 2011, alisaini mkataba katika ligi ya Bundesliga huko Ujerumani katika klabu ya VfL Wolfsburg kwa mkataba wa miaka tatu(3).Alisainiwa katika klabu ya Wolfsburg kwa ada ya € 1.5 milioni ,Iliimfanya kuwa mchezaji muhimu zaidi katika historia ya klabu ya Cracovia. [1]

PEC Zwolle[hariri | hariri chanzo]

Klich alisajiliwa kwa mkopo katika klabu ya PEC Zwolle nchini Uholanzi kwa nusu msimu na baadaye kusajiliwa kwa ada iliyoripotiwa kama 200,000,na baadaye kuripotiwa kuwa klabu yake ya Wolfsburg inamtaka.

wakati akiwa huko Zwolle alishinda Kombe la KNVB msimu wa mwaka 2013-14 mnamo Aprili 20 2014 waliwafunga Ajax 5-1 katika fainali ambayo kwa upande wake ulimpa sifa katika hatua ya mtoano katika Ligi ya Europa.[2]

Kurudi Wolfsburg[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Juni 2014 Wolfsburg walitumia chaguo lao la ukombozi kwa Klich msimu uliofuata,Alijitahidi kucheza kikosi cha kwanza na kuwaweka benchi wachezaji kama Kevin De Bruyne, Josuha Guilavogui na Luiz Gustavo kwenye nafasi ya katikati ya uwanja.

FC Kaiserslautern[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mapema Januari 2015, Klich alijiunga na klabu ya FC Kaiserslautern,Alisaini mkataba hadi majira ya joto mwaka 2018. Ada ya kuhamishwa haikuripotiwa.

FC Twente[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 26 Agosti 2016, iliripotiwa kuwa alijiunga katika klabu ya Eredivisie FC Twente kwa mkataba wa miaka tatu. Alipewa jezi nambari 43 na kucheza katika kikosi cha kwanza katika klabu ya FC Twente mnamo 10 Septemba 2016 dhidi ya SC Heerenveen.

Alifunga goli lake la kwanza katika Klabu hiyo mnamo 2 Oktoba 2016, katika mechi ambayo walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Heracles Almelo na kuisaidia FC Twente kumaliza katika nafasi ya saba.

Leeds United[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kutoka Twente mnamo 23 Juni 2017, Klich alisaini mkataba wa miaka mitatu katika klabu ya Uingereza Leeds United kwa ada isiyojulikana. Tarehe 9 Agosti, alicheza kikosi cha kwanza katika ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Port Vale.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "New Wolfsburg signing Mateusz Klich feels equal to his new teammates | Goal.com"
  2. "Dutch Cup final: Fireworks hold up PEC Zwolle win"
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mateusz Klich kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.