Matías Almeyda
Matías Jesús Almeyda (matamshi ya Kihispania alizaliwa tarehe 21 Desemba 1973) ni kocha wa soka wa kulipwa kutoka Argentina na mchezaji wa zamani. Kwa sasa ni kocha mkuu wa klabu ya Sevilla inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).[1][2]
Anajulikana kwa jina la utani El Pelado (“kipara”) licha ya kuwa kwa muda mrefu alikuwa na nywele ndefu. Alicheza kama kiungo wa ulinzi, na sehemu kubwa ya taaluma yake aliitumia katika klabu ya River Plate pamoja na klabu mbalimbali nchini Italia, ambako aliwahi kuichezea timu nne tofauti.
Almeyda aliwakilisha timu ya taifa ya Argentina na kushiriki katika Kombe la Dunia mara mbili. Baada ya kustaafu kucheza soka mwaka 2011, alianza kazi ya ukocha akiwa River Plate, kisha Banfield, Guadalajara, San Jose Earthquakes, na baadaye AEK Athens. Akiwa AEK, alifanikiwa kushinda ubingwa wa ligi ya ndani ya Ugiriki na Kombe la Taifa (double) mwaka 2023, kabla ya kuondoka klabuni hapo Mei 2025. Mwezi uliofuata, alitangazwa rasmi kuwa kocha wa klabu ya Sevilla kwa mkataba wa miaka mitatu.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Condò, Paolo (17 Oktoba 1999). "Una Lazio mostruosa" [Monster Lazio]. La Gazzetta dello Sport (kwa Kiitaliano). Iliwekwa mnamo 30 Oktoba 2017.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Newman, Blair (30 Machi 2015). "How Sven-Goran Eriksson's Lazio won the great Serie A title race of 1999–2000". The Guardian. Iliwekwa mnamo 30 Oktoba 2017.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Brescia boosted by Almeyda". UEFA. 24 Agosti 2004. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Julai 2012. Iliwekwa mnamo 6 Desemba 2010.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Matías Almeyda kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |