Kipanya matiti-mengi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mastomys)
Kipanya matiti-mengi
Kipanya matiti-mengi wa kawaida (Mastomys natalensis)
Kipanya matiti-mengi wa kawaida (Mastomys natalensis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Murinae (Wanyama wanaofanan na vipanya-miiba)
Jenasi: Mastomys
Thomas, 1915
Ngazi za chini

Spishi 8:

Vipanya matiti-mengi ni wanyama wagugunaji wa jenasi Mastomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae walio na matiti mengi kuliko panya wote wengine. Wanatokea katika savana, nusu-jangwa na msitu|misitu]] kavu ya Afrika kusini kwa Sahara.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Wanyama hawa wanafanana na panya wa kawaida (jenasi Rattus) lakini ni wadogo zaidi. Urefu wa mwili ni sm 6-17, urefu wa mkia ni sm 5-15 na uzito ni g 12-70. Manyoya ni mafupi na mororo yenye rangi ya kahawia au kijivu mgongoni na kijivu au nyeupe tumboni. Majike wana matiti mengi kuliko panya wengine: 10-24 kulingana na spishi.

Wanatokea katika maeneo kavu na hukiakia usiku. Wanalala katika viota vya mimea kavu wanayojenga katika nyufa za miamba, chini ya mizizi ya miti, chini ya miti iliyoanguka au katika vishimo. Hula mbegu, matunda, nyasi na invertebrata wadogo, na pengine nyama mbichi ya mizoga au kutoka nyumba (kipanya matiti-mengi wa kawaida).

Kwa kawaida majike huzaa mikumbo miwili kwa mwaka, pengine 3-4. Kuna wachanga 6-12 kwa mkumbo kwa kawaida, lakini wachanga wanaweza kuwa hadi 22. Mimba huchukua karibu siku 20.

Kipanya matiti-mengi wa kawaida na yule wa kusini (M. natalensis na M. coucha) huishi katika majengo mara nyingi na wanaweza kuwa wasumbufu wabaya. Hata wanaweza kuenea magonjwa, tauni hasa. Yule wa kawaida ni hazina muhimu ya virusi ya Lassa.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]