Nenda kwa yaliyomo

Massa Candida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Massa Candida (walifariki 253-260[1]) ni jina la kundi la Wakristo 300 hivi wa karne ya 3 waliofia dini yao huko Utica kwa kuwa walikataa kutoa sadaka ya ubani kwa miungu ya Roma kama walivyoagizwa na gavana Galerius Maximus, mwakilishi wa serikali ya Dola la Roma.

Wakiwa waaminifu kwa askofu wao Kwadrato, walikabili kifodini kwa kumkiri pamoja Yesu Kristo, Mwana wa Mungu[2].

Jina linatokana na jinsi walivyouawa kwa kutupwa katika shimo la chokaa hai na hivyo kugeuka rundu la vumbi jeupe [3].

Sifa yao imedumishwa na maandishi ya Agostino wa Hippo na Prudentius.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yako huadhimishwa tarehe 18 Agosti[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1.  "Massa Candida". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/92896
  3. Among other torments, the governor ordering a limekiln to be lighted and live coals with incense to be set near by, said to these confessors of the Faith: "Choose whether you will offer incense to Jupiter or be thrown down into lime." And they, armed with faith, confessing Christ, the Son of God, with one swift impulse hurled themselves into the fire, where in the fumes of the burning lime, they were reduced to a powder. Hence this band of blessed ones in white raiment have been held worthy of the name, White Mass.
  4. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.