Mauaji ya Mpeketoni
Mauaji ya Mpeketoni yalitokea kati ya tarehe 15 na 17 Juni mwaka wa 2014, ambapo zaidi ya watu 60 waliuawa katika mashambulizi eneo la Mpeketoni na viunga vyake nchini Kenya. Kundi la wanamgambo la Al-Shabaab lenye makao yake nchini Somalia lilidai kuhusika, lakini aliyekuwa Rais wa Kenya wakati huo Uhuru Kenyatta alidai kwamba mashambulizi hayo yalipangwa na wanasiasa wa eneo hilo waliokuwa na uhusiano na makundi ya uhalifu. Waandishi wa habari kutoka eneo hilo hata hivyo walidai kuwa huenda mashambulizi hayo yalichochewa na chuki za kikabila au kidini au ulipizaji wa kisasi dhidi ya unyakuzi wa ardhi.
Shambulizi la kwanza
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 15 Juni 2014, watu 50 waliokuwa wamejihami kwa bunduki huku wakiwa wamejifunika nyuso zao, waliteka nyara gari [1] na kuvamia kituo cha polisi katika kijiji cha Mpeketoni, Kenya kilicho na wakristo wengi [2] Kulingana na polisi, watu hao waliokuwa wamejihami waliwapiga risasi wanaume kiholela huku wanawake wakilazimishwa kutazama. [1] Washambuliaji hao pia walichoma hoteli, mikahawa na ofisi za serikali. [3]
Kulingana na aliyekuwa Raisi wa Kenya wakati huo Uhuru Kenyatta, idara ya polisi eneo hilo la Mpeketoni walipokea onyo la shambulizi hilo mapema, lakini hawakufanyia kazi onyo hilo. [4] Hakuna hata polisi mmoja aliyekuwa zamu kazini wakati wa shambulizi hilo aliuwawa huku kikosi cha wanajeshi waliokuwa takriban kilomita 30 (mi 19) kutoka kijiji hicho hawakufika mapema hadi takriban saa 10 baada ya shambulizi hilo, na kusababisha gazeti la The Standard kutangaza kuwa "serikali iliuza watu wake kwa washambuliaji hao". Uchunguzi uliofanywa na gazeti hilo ulisema kuwa polisi walipuuza wito wa usaidizi, na hata kuzima radio zao,huku wengine walikuwa wakitazama kandanda Kombe la Dunia na hawakupokea taarifa kuhusu shambulizi hilo.Walioshuhudia walisema waliambiwa kuwa magari ya polisi hayakuwa na mafuta ya kutosha kufika eneo la tukio ili kusaidia.Kamishna wa polisi, ambaye aliripotiwa kusimamishwa kazi baada ya shambulizi hilo, alisema "Tulijibu shambulizi hilo vilivyo lakini tulizidiwa na nguvu." [5]
Baada ya mashambulizi hayo, wenyeji waliojawa na hasira waliandamana katika barabara za kijiji cha Mpeketeni. [6]
Takriban watu 53 waliripotiwa kuuawa kwenye shambulizi hilo huku watu 8 hawakujulikana waliko kufikia Juni 18. [4] Watu wengi walioaga dunia kwenye shambulizi hilo walikuwa wa jamii ya Wakikuyu . [6]
Shambulizi la pili
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 17 Juni 2014, washambuliaji walichoma moto nyumba katika vijiji vya Majembeni na Poromoko, karibu na Mpeketoni. Ripoti za awali zilisema wanawake kumi na wawili walitekwa nyara wakati wa uvamizi huo, lakini baadaye ilithibitishwa kuwa sio ukweli.[4]
Baada ya shambulizi la pili, idara ya usalama ilikama kundi la washukiwa ambao walikuwa wamejihami na bunduki aina AK-47 waliokuwa wakitoroka kijiji hicho cha Mpeketoni. Washukiwa watano waliuwawa kwa kupigwa risasi kwenye mashambulizi baina yao na polisi huku wengine wakitoroka. [6]
Wahusika
[hariri | hariri chanzo]Japo hakuna kundi lolote lililodai kuhusika kwenye shambulizi la kwanza, msemaji wa jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir alisema "kuna uwezekano mkubwa waliotekeleza shambulizi hilo lilikuwa kundi la Al-Shabaab ". [7]
Hata hivyo kundi la Alshabaab lilidai kuhusika kwenye shambulizi la pili, wakidai kuwa waliuwa watu 20. Raisi Uhuru Kenyatta alidai kuwa baadhi ya wanasiasa wa eneo hilo walikuwa na uhusiano na kundi hilo la kigaidi na kuchochea mashambulizi hayo huku akipuuzilia mbali madai ya kundi la Alshabaab kuhusika. [6]
Wenyeji wa eneo hilo waliishtumu serikali kwa kujaribu kuipatia jamii ya wakikuyu ardhi.Malalamiko hayo yakichochewa zaidi na ghasia za kikabila kufuatia matokea ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 uliokumbwa na mzozo.Raisi Uhuru Kenyatta ambaye ametoka jamii ya wakikuyu alisema mashambulizi hayo yalichochewa kisiasa dhidi ya kabila fulani kwa lengo la kuwafurusha.Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alikuwa ameshindwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2013 na raisi Uhuru Kenyatta alikanusha kuhusika kwenye ghasia hizo na kusema matamshi ya Kenyatta hayakuwa ya haki na ukweli wowote
Hata hivyo baadhi ya waandishi wa habari kutoka eneo hilo walidai mashambulizi hayo huenda yalichochewa kikabila kati ya jamii ya Wasomali na Waoromo na kusingizia kundi la Al-Shabaab kwa kutumia bendera yao.
Tarehe 25 Juni, Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy alikamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na shambulizi hilo.
- 1 2 Gander, Kashmira (16 Juni 2014). "Kenya hotel attack: Suspected al-Shabaab militants kill 48 people in Mpeketoni". The Independent. Iliwekwa mnamo 16 Juni 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Unidentified gunmen hit hotels, petrol, police station at Kenya's coast: police". Reuters. 16 Juni 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑
{{cite news}}: Empty citation (help) - 1 2 3 "Kenya attacks: Al-Shabab raid village near Mpeketoni". BBC News. 17 Juni 2014. Iliwekwa mnamo 17 Juni 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑
{{cite news}}: Empty citation (help) - 1 2 3 4 "Kenya attack: Five suspects shot dead near Mpeketoni". BBC News. 19 Juni 2014. Iliwekwa mnamo 19 Juni 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "'Islamists' attack Kenyan town near Lamu killing 48". BBC News. 16 Juni 2014. Iliwekwa mnamo 16 Juni 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)