Maryknoll
Maryknoll ni jina la mashirika ya Kanisa Katoliki kutoka nchini Marekani. Jina limetokana na seminari ya kufunza mapadre iliyoanzishwa mwaka 1920 iliyoitwa kwa heshima ya Bikira Maria "Mary´s Knoll".
Shabaha yake ni uenezaji wa imani ya Kikristo katika nchi za misheni. Jumuiya hiyo huwa na mashirika matatu: moja la mapadri na mabruda wa Maryknoll (The Catholic Foreign Mission Society of America), moja la masista wa Maryknoll na moja la walei (Maryknoll Lay Missioners).
Jumuiya ilianzishwa na mapadre wawili, Thomas F. Price na James A. Walsh mjini Hawthorne katika jimbo la New York (jimbo) ikathibitishwa tarehe 29 Juni 1911 na Papa Pius X.
Wamisionari wa Maryknoll wamefanya kazi huko Asia ya Mashariki (China, Japani, Korea), Amerika ya Kilatini na Afrika.
Makao makuu ya Maryknoll yako Ossining, Westchester County, New York.
| Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maryknoll kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |