Mary Lazarus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mary Lazarus Alizaliwa tarehe 5 Mei , 1989)[1] ni mwigizaji wa kike wa Nigeria na mtayarishaji wa filamu ambaye alishinda tuzo ya City People Movie Award for Most Promising Actress of the Year (English) kwenye Tuzo za Burudani za Watu wa Jiji mwaka 2018 [2] na alitajwa kwenye kinyang'anyiro cha Best Actress in a leading role katika mwaka huohuo kwenye Best of Nollywood Awards.[3]

Maisha ya awali na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Lazarus ametokea katika Jimbo la Abia lililopo Nigeria, Ambalo lipo kusini-mashariki mwa Nigeria ambapo mwanzo walikuwako watu wa Igbo wa Nigeria. Lazarus ametokea katika serikali ya mtaa wa Ukwa Mashariki ya jimbo la Abia na alizaliwa katika familia ya watu tisa ukimjumuisha mama, baba na wadogo wake sita ambapo ni pacha na mmoja wa watoto wa mwisho katika familia pamoja na pacha wake wakiume aitwaye Joseph.[4] Lazarus alipata elimu ya msingi na sekondari na alipata cheti chake cha kwanza cha kumaliza na cheti cha shule ya West African Senior pia alituma maombi ya kujiunga na chuo cha Ibadan.Alikubaliwa na kusoma shahada ya Jiografia katika chuo hicho.[5][6]

kazi[hariri | hariri chanzo]

Lazarus anayefahamika kwa uhusika mbalimbali filamu za Nollywood aliingia kwa mara kama mwanamitindo mnamo mwaka 2002 kabla ya kuingia rasmi katika tasnia ya filamu ya Nigeria mwaka 2009 katika filamu iliyojulikana kama “Waiting Years” alipata uhusika huu kwa msaada wa Gbenro Ajibade aliyemtambulisha kwa John Njamah, muongozaji wa filamu hiyo .[7] Lazarus alifanya kazi uyake ya kwanza kama muongozaji katika filamu iliyojulikana kwa jina la “Dance To My Beat” iliyotolewa mwaka 2017.

Lazarus kama mwanamitindo ametokea katika matangazo ya kibiashara ya Airtel Africa|Airtel na MTN Group MTN.[8][9]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Mary Lazarus 5 Nollywood movies featuring actress". www.pulse.ng. Iliwekwa mnamo 2019-12-23. 
  2. People, City (2018-09-24). "Winners Emerge @ 2018 City People Movie Awards". City People Magazine (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-12-23. 
  3. "BON Awards 2018: Mercy Aigbe, Tana Adelana shine at 10th edition". Pulse Nigeria (kwa en-US). 2018-12-09. Iliwekwa mnamo 2019-12-23. 
  4. "Actress Mary Lazarus And Twin Brother Celebrate Birthday Today (Pictures) – Nairaland". Nigeria News (News Reader) (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-23. 
  5. "8 Things you should know about the starlet". Pulse Nigeria (kwa en-US). 2015-08-17. Iliwekwa mnamo 2019-12-23. 
  6. Published. "Many misuse social media –Mary Lazarus". Punch Newspapers (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-12-23. 
  7. Published. "Modelling prevented me from making a first-class degree — Mary Lazarus". Punch Newspapers (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-12-23. 
  8. "Mary Lazarus implores government to build cinema housesdate[[2018-06-20]]website=Vanguard News" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-12-23.  Wikilink embedded in URL title (help)
  9. Legit.ng (2012-10-05). ""Every Part Of My Body Is Sexy"- Actress Mary Lazarus". www.legit.ng (kwa Kiingereza).  Unknown parameter |access-date2019-12-23accessdate2020-12-19archiveurl= ignored (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mary Lazarus kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.