Nenda kwa yaliyomo

Marwa Arafa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

{{{{wikigapjwk2026}}}} Marwa Arafa ni mwanaharakati wa haki za watoto na mtafsiri kutoka Misri. Alikamatwa na kutoweka mikononi mwa polisi wa Misri mnamo Aprili 2020.[1][2] Alishtakiwa kwa kujiunga na shirika la kigaidi na alizuiliwa kwa miaka miwili bila kufunguliwa mashtaka.

Kukamatwa na kutoweka kwa lazima

[hariri | hariri chanzo]

Arafa ni mwanachama wa shirika la Ukombozi wa Watoto ambalo linatetea uhuru wa watoto waliofungwa.[3] Mnamo Aprili 2020, maafisa wa usalama wa serikali ya Misri walivamia nyumba yake, wakafanya upekuzi na kumkamata bila kuwa na hati ya upekuzi wala ya kukamatwa.[4] Alitoweka kwa siku 14 bila kuwa na dalili yoyote ya kuonekana. Mnamo Mei 2020, maafisa wa usalama walimwasilisha pamoja na hati cha kukamatwa katika ofisi ya Mashtaka ya Usalama wa Kitaifa ambapo alipewa Kesi Nambari 570 na kuhojiwa.[5][2]

Arafa alishtakiwa kwa kujiunga na kufadhili shirika la kigaidi. Baadaye aliwekwa kizuizini kwa miaka miwili zaidi ya muda ulioruhusiwa kisheria. Alivyokuwa kizuizini, binti yake mwenye umri chini ya miaka mitatu alikataliwa kumwona mama yake.[6]

  1. esa (2022-06-08). "#FreeMarwaArafa - Regional Coalition of WHRDs" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
  2. 1 2 Ihor Andriichuk (2022-02-24). "Two translators are still detained in Egypt". Endangered Scholars (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
  3. Omar Odeh. "When helping people in need is a crime: The case of Marwa Arafa". Mada Masr (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
  4. "Egypt forcibly disappears two women amid coronavirus crackdown: Rights group - AL-Monitor: The Middle Eastʼs leading independent news source since 2012". www.al-monitor.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
  5. "Rights group calls on Egypt to release two disappeared women". Al Jazeera (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
  6. "Mother of 2-year-old forcibly disappeared in Egypt". Middle East Monitor. 2020-04-22. Iliwekwa mnamo 2026-01-30.