Nenda kwa yaliyomo

Mimbari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Marufaa)
Mimbari katika kanisa la Kipresbiteri huko California (Marekani).
Mimbari ya Kikatoliki huko Almenno San Salvatore (Bergamo, Italia).

Mimbari (au "marufaa" kutoka maneno ya Kiarabu; pia "ambo", kutoka jina la Kilatini) ni mahali pa kutangazia Neno la Mungu katika maabadi ya dini mbalimbali.

Umuhimu wake unatofautiana kadiri ya dini na ya madhehebu husika. Kwa mfano, upande wa Ukristo, katika Uprotestanti inashika nafasi ya kwanza ndani ya kanisa, wakati Ukatoliki unapendelea altare inapotolewa sadaka ya ekaristi, ingawa unataka sehemu hizo mbili zilingane kwa kuwa ni meza mbili ambapo Mungu anawalisha wanae kwanza Neno, halafu Mwili na Damu ya Kristo.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.