Martha Isabel Ruiz Corzo

Martha Isabel "Pati" Ruiz Corzo (alizaliwa Mexico City, 17 Januari 1953) ni mwanamazingira nchini Meksiko. Ndiye mwanzilishi wa kundi la Ekolojia la Sierra Gorda, ambalo limefanikiwa kuongoza juhudi za mashinani za kuhifadhi Sierra Gorda katikati mwa Meksiko tangu mwaka 1987. Mnamo mwaka 2013, alitajwa kuwa bingwa wa dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP).
Maisha ya Awali na Binafsi
[hariri | hariri chanzo]Martha Isabel Ruiz Corzo alilelewa katika familia tajiri huko Santiago de Querétaro katika jimbo la kati la Meksiko la Querétaro.[1] Yeye mara nyingi huitwa kwa jina la "Pati", jina la utani linalotokana na jinalake la utotoni "pata" ambalo dada yake alimwita.[1] Pati alianza kupiga fiyoli akiwa na umri wa miaka 12, na alipokuwa kijana, akawa mpiga fiyoli wa kwanza katika Orkestra ya Querétaro Philharmonic, nafasi ambayo alishikilia kwa miaka mitano.[1][2] Kwa miaka 16, alifundisha muziki katika Shule ya John F. Kennedy huko Querétaro.[3] Aliolewa na mwanauchumi anayetwaye kwa jina la Roberto Pedraza Muñoz (aliyezaliwa 1950) na kupata watoto wawili wakiume wanaokwenda kwa majina ya Roberto ("Beto") na Mario.[2][4]
Hata hivyo, Ruiz Corzo hatimaye alianza kuchoshwa na maisha ya kisasa ya jiji. Alihusisha matatizo ya afya ya familia yake na uchafuzi wa mazingira mijini na alisema alijihisi "kuzibwa pumzi" na kanuni za kijamii la tabaka la juu.[5][6]Akitafuta maisha mazuri, familia ya Pedraza Ruiz walihamia karibu na mazingira ya asili mwaka wa 1984 katika milima yenye misitu ya eneo la nyumbani la Pedraza Muñoz, linaloitwa Sierra Gorda kaskazini mwa jimbo la Querétaro.[7][8]
Taaluma ya mazingira
[hariri | hariri chanzo]Ruiz Corzo alikuja kujulikana kwa harakati zake za kuhifadhi mfumo wa ikolojia wenye aina nyingi za viumbe wa Sierra Gorda. Kufikia miaka ya 1980, eneo hilo lilikuwa likitishiwa na shughuli za uchimbaji madini, ukataji miti ovyo, uwindaji haramu, utapaji taka hovyo, uchafuzi wa maji, moto wa misitu usiodhibitiwa, na changamoto nyingine nyingi.
Mnamo mwaka 1987, Ruiz Corzo na mumewe Pedraza Muñoz walianzisha shirika lisilo la kiserikali linaloitwa , Kikundi cha Ikolojia cha Sierra Gorda (GESG, Grupo Ecológico Sierra Gorda), ili kukuza uendelevu katika eneo hili.[3][5] Kikundi hiki kwanza kililenga kuongeza uhamasishaji katika shule za Sierra Gorda, kilifanya matukio ya elimu ya mazingira yaliyohusisha jukwaa la maigizo na muziki, yakiwemo nyimbo na uchezaji wa akodioni wa Ruiz Corzo mwenyewe.[1] Baada ya muda, kwa kupata mvuto mkubwa wa utu na uongozi wa Ruiz Corzo, GESG ilitoa usaidizi mashinani ya mazingira kama vile usafishaji, upandaji miti upya na kadhalika miongoni mwa jamii ya watu wa pato la chini eneo la Sierra Gorda.[1][5] Nuestra Tierra ("Ardhi Yetu") ni kipindi cha redio cha kikundi, kilichorushwa hewani kwa mara ya kwanza mwaka 1990.[9] Kadri kikundi kilipokua, kilivutia uungwaji mkono kutoka kwa Gavana wa Querétaro anayeitwa Enrique Burgos García na kupata ufadhili wa kifedha kutoka kwa vikundi vingi vya kimataifa, kama vile Shirika la Ulimwengu la Ardhi na Mfuko wa Kimataifa wa Mazingira.[1][4]
GESG iliomba kwa miaka mingi Sierra Gorda itambuliwe kama hifadhi ya viumbe hai. Hatimaye ilifanikiwa mnamo mwezi Mei 1997, wakati rais wa Meksiko Ernesto Zedillo alipoanzisha Hifadhi ya Mazingira ya Sierra Gorda zaidi ya hekta 385,000 (ekari 950,000) za ardhi, theluthi moja ya jimbo la Querétaro.[3][7] Hii iliipa wizara ya mazingira ya Meksiko mamlaka ya kulinda aina mbalimbali za mazingira katika eneo hilo.[9] Ruiz Corzo alihudumu kama mkurugenzi wa uzinduzi wa hifadhi kwa miaka 14.[1][2] Kama mkurugenzi, alisaidia kuweka fidia kwa wenyeji wanaolinda mfumo ikolojia wa ardhi yao badala ya kuutumia kwa shughuli kama vile kilimo cha kujikimu.[4][10] Ruiz Corzo mara nyingi alipigania maslahi ya kibinafsi na ya umma kama vile kampuni ya kitaifa ya umeme, ambayo ilitaka kupanua njia za umeme katika hifadhi licha ya marufuku katika eneo lililohifadhiwa.[1][4]
Kufikia 2023, GESG inaendelea kusaidia kufadhili na kutetea uhifadhi katika nyanja nyingi, kama vile ukataji miti endelevu, udhibiti wa taka, usimamizi wa udongo, utalii wa mazingira, na elimu.[7] Mojawapo ya mipango ya GESG leo inatoa mafunzo kwa walimu kufikia zaidi ya wanafunzi 15,000 katika eneo hili kila mwaka. Ruiz Corzo alianza tena kuongoza GESG mwaka wa 2009, na anaendelea kufanya kampeni katika ngazi za ndani, kitaifa na kimataifa.[3][5] Jarida linalokwenda kwa jina la The Ecologist liliandika mwaka wa 2016 kwamba Ruiz Corzo "anaweza kuzungumza na hadhira kubwa bila woga na karibu kila mara anamalizia hotuba kwa kuimba".[5]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Mashirika mbalimbali yamemtambua Ruiz Corzo kwa uanaharakati wake, ikijumuisha tuzo mbili kutoka vitengo vya Umoja wa Mataifa: Mashujaa wa Dunia (2013, kutoka UNEP) na tuzo ya Wangari Maathai ya Mashujaa wa Misitu(2014, kutoka UNFF).[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 5 6 7 8 Teresa de Miguel (2022-07-14). "La maestra de música que protegió los bosques de Querétaro a golpe de acordeón". El País México (kwa Mexican Spanish). Iliwekwa mnamo 2025-10-06.
- 1 2 3 "Welcome to ONE WORLD AWARD". www.one-world-award.com (kwa Kijerumani). Iliwekwa mnamo 2025-10-06.
- 1 2 3 4 5 "The Team – Grupo Ecológico Sierra Gorda IAP" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-10-06.
- 1 2 3 4 Pastrana, Daniela (2010-07-05), "Conservation can be a weapon against poverty", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2025-10-06
- 1 2 3 4 5 "Activist 'Pati' Ruiz Corzo: The Singing Conservationist". theecologist.org (kwa Kiingereza). 2016-08-25. Iliwekwa mnamo 2025-10-06.
- ↑ DEMOS, Desarrollo de Medios, S. A. de C.V (2012-07-22). "La Jornada: El premio National Geographic 2012, para Paty Ruiz Corso y la sierra de Querétaro". www.jornada.com.mx (kwa Mexican Spanish). Iliwekwa mnamo 2025-10-06.
{{cite web}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - 1 2 3 "Women building a sustainable future: The Mexican violinist who saved the Sierra Gorda | UN News". news.un.org (kwa Kiingereza). 2022-02-06. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-02-10. Iliwekwa mnamo 2025-10-06.
- ↑ EST, Published 7:37 PM; January 28, Thu; 2021 (2021-01-29), Meet the guardian of Mexico’s ‘fat mountains’ | CNN (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2025-10-06
{{citation}}:|last3=has numeric name (help)CS1 maint: numeric names: authors list (link) - 1 2 Por Gonzalo Soto (2018-07-25). "Ella es la mujer que salvó la Sierra Gorda de Querétaro". El Financiero (kwa Kihispania). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-02-11. Iliwekwa mnamo 2025-10-06.
- ↑ U. N. Environment (2019-08-22). "Martha Isabel Ruiz Corzo | Champions of the Earth". www.unep.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-06.