Marlie Packer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marlie Packer

Marlie Packer (alizaliwa 2 Oktoba 1989) ni mchezaji wa raga wa Uingereza (safu ya nyuma / beki) kwenye timu ya Saracens na timu ya wanawake ya Uingereza. Alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda Kombe la Dunia la Raga la Wanawake la 2014.[1]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Packer alianza kazi ya uchezaji wa kimataifa akiichezea Uingereza mwaka 2008. Mnamo 2013, alichezea kikosi cha Uingereza kwenye Mchezo wa Saba wa Kombe la Dunia la Raga ya Wanawake 2013 huko Moscow. Aliendelea kuchezea timu ya Uingereza ya walio na umri chini ya miaka 15 iliyoshinda Kombe la Dunia la 2014, na tena katika Kombe la Dunia la Raga ya Wanawake ya 2017 [2].

Ameshinda mataji manne ya Mataifa sita ya Grand Slam akiwa na Uingereza hadi sasa. Packer alianza mechi zote isipokuwa moja kati ya mechi za Uingereza za 2019 za Rugby Super Series na alipewa kandarasi ya muda wote ya kucheza katika timu ya Uingereza mwaka wa 2019. Mnamo 2020, jeraha la kifundo cha mguu lilimzuia kucheza michuano ya Mataifa Sita ya mwaka huo.[3]

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

  • 2014 Mshindi wa Kombe la Dunia la Raga ya Wanawake
  • 2014 Freedom of Yeovil
  • 2017 Mshindi wa fainali ya Kombe la Dunia la Raga ya Wanawake

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Alison Donnelly (Scrum Queens) (July 2014). "England name WC squad". Iliwekwa mnamo 20 August 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "RFU". www.englandrugby.com. Iliwekwa mnamo 2021-04-21. 
  3. "England Women without Marlie Packer for 2020 Six Nations campaign". Sky Sports (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-21. 
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marlie Packer kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.