Nenda kwa yaliyomo

Marian Ewurama Addy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Marian Ewurama Addy FGA OV (née Cole; 7 Februari 1942  Januari 14, 2014) alikuwa mwanabiolojia wa kutoka nchini Ghana [1] [2] [3] na mwenyeji wa kwanza wa Jaribio la Kitaifa la Sayansi na Hisabati . [4] [5] [6] Mwanamke wa kwanza wa Ghana kufikia cheo cha ngazi ya profesa kamili wa sayansi asilia, Addy akawa mfano wa kuigwa kwa wasichana wa shule na wanasayansi wanawake chipukizi kwenye fursa zisizo na kikomo ndani ya taaluma za sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM). [7] [8] Pamoja na hayo Marian Addy pia alikuwa Mwanachama wa Chuo cha Sanaa na Sayansi cha Ghana, aliyeteuliwa mnamo wa 1999. [9] [7] Katika mwaka huo huo, alipewa Tuzo ya UNESCO Kalinga kwa Uenezaji wa Sayansi. [9]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Marian Ewurama Cole alizaliwa mnamo wa 7 Februari 1942 huko Nkawkaw kwenye Mkoa wa Mashariki wa Ghana, kwa Samuel Joseph Cole na Angelina Kwofie Cole. [10] [9] Alisoma elimu ya sekondari kwenye Shule ya Sekondari ya St Monica huko Mampong-Ashanti kuanzia tarehe ya Januari 1956 hadi Juni 1960 ambapo alifaulu katika michezo na kupata vyeti vyake vyakidato cha 4 na kidato cha 6 . [11] Alifanikiwa pia alihudhuria Shule ya Wasichana ya Holy Child huko Cape Coast . Alitunukiwa Shahada yake ya Kwanza na heshima ya daraja la kwanza juu ya botania na kemia kutoka Chuo Kikuu cha Ghana, Legon . Kisha Baadaye alipata shahada ya uzamili na udaktari katika biokemia kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Pennsylvania . [12] [13]

Addy alipata cheo cha profesa kamili wa biokemia ndani ya Chuo Kikuu cha Ghana, mahali ambapo hakuwa tu profesa wa kwanza mwanamke katika sayansi katika chuo kikuu tu, lakini ni pamoja na nchini nzima ya Ghana kiujumla. [12] [14] Kwenye chuo kikuu hicho hicho, alipata nafasi ya kuwa Mkuu wa Idara ya Biokemia, Biolojia ya Seli na Molekuli kuanzia mwaka 1988 hadi 1991 na mwaka 1994 hadi 1997. Addy alistaafu mwaka wa 2002 kama Profesa wa Biokemia. [14]

Kwenye enzi zake kama profesa na mkuu wa idara, alikuwa pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Sera ya Nchi Zinazoendelea (PCDC) na alisimamia Bodi ya Kitaifa ya Mitihani ya Kitaalamu na Mafundi (NABPTEX) . Aliongoza kama mkurugenzi wa programu ya Programu ya Elimu ya Sayansi kwa Afrika (SEPA) yenye makao yake Accra, programu ya elimu ya sayansi ya awali ya chuo kikuu ya Pan African katika miaka ya 1970. [12] Alifanya kazi kwenye Kamati ya Kwami, kamati ya kiufundi ya elimu ya polytechnic iliyotengenezwa na Baraza la Kitaifa la Elimu ya Juu (NCTE), ili kusoma na kuelezea sera za kusaidia serikali ya Ghana kwenye kusaidia elimu ya polytechnic. [15]

Mwaka wa 1994, alikuwa mshirika wa timu ya washauri ya UNDP yenye wanachama 4 nchini Ghana iliyopewa jukumu la kuunda Programu ya Kitaifa ya Utekelezaji wa Sayansi na Teknolojia. [16] Alifanikiwa kuwa mjumbe wa bodi ya Tume ya Nishati ya Atomiki ya Ghana kuanzia mwaka 1996 hadi 1998. [17] Alifanya kazi kama mjumbe wa Kamati ya Wataalamu wa Kikanda ya WHO juu ya Tiba ya Jadi, na alifanya kazi kama mshauri wa Wakfu wa Kimataifa wa Sayansi, huko eneo la Stockholm, Sweden . [7] Alikuwa Mwanzilishi na Katibu Mtendaji wa Kwanza wa Mtandao wa Wanasayansi wa Utafiti wa Bidhaa Asili wa Afrika Magharibi (WANNPRES), ambao ulianzishwa mnamo Februari 2002. [12]

Alikuwa na uzoefu mkubwa kwenye sayansi ya msingi na sayansi inayotumika, akitoa masomo kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza, shahada ya uzamili, meno na udaktari ndani ya Chuo Kikuu cha Ghana, Legon na hapo baadaye katika Chuo cha Tiba cha Chuo Kikuu cha Howard huko Washington DC . [7] [18]

Mwaka wa Januari 2008, Addy alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Anglikana, mpango wa teknolojia kwenye elimu ya juu.

Kifo na urithi

[hariri | hariri chanzo]

Alifariki dunia kutokana na sababu za kawaida tarehe 14 Januari 2014 katika Hospitali ya Mafunzo ya Korle-Bu huko Accra. [19] [20] Mwili wake ulipata mazishi tarehe 1 Machi 2014 huko Saltpond, mji wa kihistoria wa pwani katika Mkoa wa Kati wa Ghana . [21] Maabara ya sayansi kwenye Idara ya Biokemia, Biolojia ya Seli na Molekuli ndani ya Chuo Kikuu cha Ghana, iliitwa " Maabara ya Marian Ewurama Addy ya Utafiti wa Mimea ya Dawa na Bidhaa za Asili " kwa heshima yake. [22] Pamoja na Idara ya biokemia ilianzisha Hotuba ya Ukumbusho ya Profesa Marian Ewurama Addy ya kila mwaka kwa kumbukumbu zake . [23] Kazi yake ya utafiti juu ya biokemia ya dawa ya bidhaa za mitishamba ilisibabisha dawa za mitishamba kujulikana zaidi na kukubalika kwa jamii ya kisayansi. Jaribio la Kitaifa la Sayansi na Hisabati bado hufanyika kila mwaka na linaendelea kuleta sayansi mbele ya mawazo ya umma na kukuza hesabu na sayansi kwa watoto wadogo. [24]

Tuzo na heshima

[hariri | hariri chanzo]
  • Tuzo ya Shell, iliyotolewa na Kampuni ya Shell, Ghana Ltd, kwa wagombea sita bora waliofaulu Cheti cha Mitihani cha Jumla, "A", 1962 [13]
  • Tuzo ya McCallien, iliyotolewa kwa mwanafunzi bora zaidi katika Volta Hall, ukumbi wa makazi wa kike, 1963 [13]
  • Tuzo ya Waddell, iliyotolewa kwa mwanafunzi bora wa sayansi, 1962–66 [13]
  • Tuzo la California, lililotolewa na Idara ya Kemia, Chuo Kikuu cha Ghana, kwa mwanafunzi bora wa mwaka wa kwanza katika Kemia, 1962–63 [13]
  • Mwanachama, Programu ya Ushirika wa Wahitimu wa Kiafrika (AFGRAD) wa Taasisi ya Waamerika Weusi, 1966–71 [13]
  • Mwanachama wa Semina ya Kimataifa ya Kemia, katika Chuo Kikuu cha Uppsala, Uppsala Sweden, 1985–86 [13]
  • Tuzo la Mwanasayansi Mwandamizi wa Kiafrika la Fulbright mnamo 1990 [13]
  • Mwanamke Bora wa Mwaka wa Masoko wa CIMG, mwaka wa 1995, kwa Sayansi ya Masoko. [9]
  • Mwanafunzi Bora wa Taasisi ya Afrika-Amerika mwaka wa 1998. [25]
  • Tuzo ya UNESCO Kalinga kwa Uenezaji wa Sayansi mnamo 1999. [12]
  • Tuzo ya Ubora wa Milenia kwa Maendeleo ya Elimu mwaka wa 1999. [25]
  • Alihitimu kama Mwanachama wa Chuo cha Sanaa na Sayansi cha Ghana mnamo 1999. [7]
  • Tuzo ya Kitaifa kutoka kwa Kampuni ya Bima ya Biashara Limited wakati wa maadhimisho yao ya miaka 75 mwaka wa 1999, kwa "mchango muhimu katika kuelimisha watoto wa Ghana na kwa kujenga shauku katika Hisabati na Sayansi" [13]
  • Ufinyanzi wa asidi-amino huru [alpha] kama mfumo wa upolimishaji wa kibiolojia (1971)
  • Maonyesho ya Kijeni: Mwongozo wa Mwalimu (1980); iliyoandikwa kwa ushirikiano na Ebenezer Laing na Carol Markwei
  • Kuweka Sayansi katika Sanaa ya Uponyaji kwa Mimea: Kutoka kwa Kymograph ya Ngoma ya Kuvuta Moshi hadi ELISA (2003) [9]
  • Kufundisha Kizazi Kijacho cha Wanasayansi (2004) [26]
  • Zawadi: Tawasifu (2011) [27]
  1. "Marian Ewurama Addy" (PDF). unevoc.unesco.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 15 Januari 2014. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Marian Ewurama Addy, Professor". GhanaWeb (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-12-18. Iliwekwa mnamo 2017-07-09.
  3. Glossary on Kalinga Prize Laureates. "UNESCO Kalinga Prize Winner - 1999: Prof. Marian Ewurama Addy" (PDF).
  4. "Prof Marian Ewurama Addy passes on". myjoyonline. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Ghana News - Prof Marian Ewurama Addy laid to rest". Myjoyonline. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 1 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Ghana TV quiz promotes math and science". Public Radio International (kwa Kiingereza). 2 Agosti 2016. Iliwekwa mnamo 2019-11-30.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 1 2 3 4 5 "Marian Ewurama Addy, Professor". GhanaWeb (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-12-18. Iliwekwa mnamo 2017-07-09."Marian Ewurama Addy, Professor". GhanaWeb. Archived from the original on 18 December 2016. Retrieved 9 July 2017.
  8. "Tribute To Prof Marian Ewurama Addy". ghanadot. Iliwekwa mnamo 2017-07-09.
  9. 1 2 3 4 5 "Marian Ewurama Addy" (PDF). unevoc.unesco.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 15 Januari 2014. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"Marian Ewurama Addy" (PDF). unevoc.unesco.org. Archived (PDF) from the original on 15 January 2014. Retrieved 14 January 2014.
  10. Glossary on Kalinga Prize Laureates. "UNESCO Kalinga Prize Winner - 1999: Prof. Marian EWURAMA ADDY" (PDF).
  11. Coverghana.com.gh (2021-11-23). "Meet the first NSMQ Mistress, Prof. Marian Ewurama Addy". Coverghana (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-03-19. Iliwekwa mnamo 2023-08-17.
  12. 1 2 3 4 5 Coverghana.com.gh (2021-11-23). "Meet the first NSMQ Mistress, Prof. Marian Ewurama Addy". Coverghana (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-03-19. Iliwekwa mnamo 2023-08-17.Coverghana.com.gh (23 November 2021). "Meet the first NSMQ Mistress, Prof. Marian Ewurama Addy" Ilihifadhiwa 19 Machi 2025 kwenye Wayback Machine.. Coverghana. Retrieved 17 August 2023.
  13. 1 2 3 4 5 6 7 8 9 Glossary on Kalinga Prize Laureates. "UNESCO Kalinga Prize Winner - 1999: Prof. Marian EWURAMA ADDY" (PDF).Glossary on Kalinga Prize Laureates. "UNESCO Kalinga Prize Winner - 1999: Prof. Marian EWURAMA ADDY" (PDF).
  14. 1 2 "Late Professor Marian Ewurama Addy Honoured | University of Ghana". University of Ghana. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Desemba 2015. Iliwekwa mnamo 2019-11-30.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "Marian Ewurama Addy profile". Ghanaweb. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. "Marian Ewurama Addy profile". Ghanaweb. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"Marian Ewurama Addy profile". Ghanaweb. Archived from the original on 12 February 2015. Retrieved 12 February 2015.
  17. "Ghana Atomic Energy Commission: At a Glance" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-08-20.
  18. Busia, Kofi (2014). "Obsequies - late Prof. Marian Ewurama Addy". African Journal of Traditional, Complementary and Alternative Medicines. 11 (2): 489. ISSN 2505-0044. PMC 4202662. PMID 25435638.
  19. "Marian Ewurama Addy profile". Ghanaweb. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  20. Blackandwhitegh (2014-01-14). "Prof. Marian Ewurama Addy, First Female Professor of Science at the University of Ghana Passes on at age 72". BlackandWhiteGH. Iliwekwa mnamo 2017-07-09.
  21. "Prof Ewurama Addy to be buried March 1". Myjoyonline. (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-08-16.
  22. "Late Professor Marian Ewurama Addy Honoured | University of Ghana". University of Ghana. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-12-13. Iliwekwa mnamo 2017-07-09.
  23. "Invitation to 2nd Professor Marian Ewurama Addy Memorial Lecture | University of Ghana". University of Ghana. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Agosti 2023. Iliwekwa mnamo 2020-05-24.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  24. "Ghana TV quiz promotes math and science". Public Radio International (kwa Kiingereza). 2 Agosti 2016. Iliwekwa mnamo 2019-11-30.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"Ghana TV quiz promotes math and science". Public Radio International. 2 August 2016. Retrieved 30 November 2019.
  25. 1 2 "Marian Ewurama Addy profile". Ghanaweb. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"Marian Ewurama Addy profile". Ghanaweb. Archived from the original on 12 February 2015. Retrieved 12 February 2015.
  26. Addy, Marian Ewurama (2004). Training the Next Generation of Scientists (kwa Kiingereza). Ghana Academy of Arts and Sciences.
  27. Addy, Marian Ewurama (2011). Rewards: An Autobiography (kwa Kiingereza). African Books Collective. ISBN 9789988037826.