Nenda kwa yaliyomo

Mariamu (dada wa Musa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mariamu na mtoto Musa katika kapu.

Mariamu alikuwa dada wa Aroni na Musa, wana wa Amram na Yokebed. Aliishi katika karne ya 13 KK.

Anatajwa katika vitabu vitatu vya Biblia (Kutoka, Hesabu na Mika).

Mariamu ni mwanamke wa kwanza kuitwa "nabii" na ndiye aliyeongoza mashangilio baada ya Mungu kuangamiza Wamisri katika maji ya Bahari ya Shamu (Kutoka 15:20-21).

Wimbo wake ni kati ya maandiko matakatifu ya kale zaidi.

Katika Kurani Bikira Mariamu anatajwa kama binti Amram.

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mariamu (dada wa Musa) kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.