Nenda kwa yaliyomo

Maria al-Qibtiyya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Māriyya bint Shamʿūn (مارية بنت شمعون, anajulikana zaidi kama Māriyyah al-Qibṭiyyah au al-Qubṭiyya, yaani Maria Mkopti; alifariki 637) alikuwa mwanamke wa Misri.

Māriyya pamoja na dada yake, Sirin bint Shamun, walipelekwa kama zawadi kwa Mtume Muhammad kutoka kwa Al-Muqawqis, ambaye alikuwa gavana Mkristo wa Alexandria wakati wa utawala wa Wasasania katika eneo hilo, mwaka 628.

Kuna mjadala iwapo Māriyya aliolewa rasmi na Mtume Muhammad au aliendelea kuwa mjakazi wake. Hata hivyo, alitumia maisha yake yaliyobaki katika mji wa Madina ambako alizaa mtoto wa kiume, Ibrahim, na Mtume Muhammad. Mtoto huyo alifariki akiwa na umri wa miaka miwili.

Kwa mujibu wa mwanahistoria Al-Maqrizi, Māriyya alitoka katika kijiji cha Hebenu (ⲡⲙⲁⲛϩⲁⲃⲓⲛ, Ἀλάβαστρων πόλις Alábastrōn pólis, الحفن), kilichopo karibu na mji wa Antinoe.[1]

  1. Al-Maqrīzī. Book of Exhortations and Useful Lessons in Dealing with Topography and Historical Remains. Ilitafsiriwa na Stowasser, Karl. Hans A. Stowasser. ku. 330–331.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.