Maria Sole Ferrieri Caputi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maria Sole Ferrieri Caputi mnamo 2022

Maria Sole Ferrieri Caputi (alizaliwa 20 Novemba 1990) ni mwamuzi wa mpira wa miguu wa Italia.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Ni mtoto wa wazazi wenye asili ya Kiapulia, Ferrieri Caputi ana shahada ya kwanza katika sayansi ya siasa na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Pisa na shahada ya uzamili katika Sosholojia kutoka Chuo Kikuu cha Florence . [1] Pia ni mtafiti katika shirika la Adapt Foundation (Chama cha Mafunzo ya Kimataifa Linganishi juu ya Sheria ya Kazi na Mahusiano ya Viwanda) na mhitimu wa udaktari katika Chuo Kikuu cha Bergamo . [2]

Kazi ya uamuzi[hariri | hariri chanzo]

Alipokua katika mji wa Livorno, Ferrieri Caputi aliingia kwenye shirika la soka la AIA mwaka 2007. [3] Mnamo Novemba 2015, alichezesha mechi ya Levito – Atletico San Paolo katika ligi ya Serie D. [4]

Mnamo 2019, alichezesha mashindano ya Torneo di Viareggio na kuwa mwamuzi wa kimataifa. [5] Alichezesha mechi yake ya kwanza ya kimataifa dhidi ya Scotland - Cyprus, katika mashindando ya kufuzu kwa UEFA Women's Euro 2022 . [5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Curriculum vitae di Maria Sole Ferrieri Caputi" (DOCx). Iliwekwa mnamo 30 September 2022.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Chi è Maria Sole Ferrieri Caputi, il primo arbitro donna a dirigere una squadra di Serie A in un match di Coppa Italia". Eurosport (kwa Kiitaliano). 2021-12-15. Iliwekwa mnamo 2022-09-30. 
  3. Pacini, Andrea (2021-04-03). "Gli sproni dell'internazionale Maria Sole Ferrieri Caputi". Associazione Italiana Arbitri (kwa Kiitaliano). Iliwekwa mnamo 2022-09-30. 
  4. "Chi è Maria Sole Ferrieri Caputi, la prima donna ad arbitrare in Serie A". Il Fatto Quotidiano (kwa it-IT). 2022-09-28. Iliwekwa mnamo 2022-09-30. 
  5. 5.0 5.1 Bianchini, Chiara (2022-09-28). "Calcio, chi è Maria Sole Ferrieri Caputi, la prima donna che arbitrerà la Serie A". intoscana (kwa it-IT). Iliwekwa mnamo 2022-09-30. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria Sole Ferrieri Caputi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.