Nenda kwa yaliyomo

Margoth Escobar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Margoth Escobar (alizaliwa 1953 au 1954) ni mwanaharakati wa haki za kimazingira na asilia wa Ekuador.[1]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Margreth Escobar ni mtu mwenye asili mchanganyiko, yaani ya Hispania na Ureno. Escobar alizaliwa Puyo (pia inajulikana kama El Puyo), mji mkuu wa mkoa wa Pastaza nchini Ekuador.[2]

Uanaharakati

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 1975 Escobar, mwanamke huyu jasiri kutoka Amazonia, alipinga vikali shughuli za uchimbaji wa maliasili katika msitu wa Amazonia ulioko Ekuador.[3]

Katika mwaka huo huo alishiriki katika kuanzisha Muungano wa mkoa wa Mashirika ya wakulima ya Manabí (Union Provincial de Organizaciones Compesanias de Manabií), ambao ulihusika kwa kiasi kikubwa katika kurejesha ardhi za kilimo kwa familia kadhaa katika mkoa wa Manabí.[1]

  1. 1 2 "Margoth Escobar". Front Line Defenders (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-10.
  2. Mayuri Castro (2020-03-25). "La Fiscalía aún no resuelve denuncias por ataques a mujeres amazónicas". GK (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 2025-10-10.
  3. José María León Cabrera (2019-04-23). "El rostro de la resistencia". GK (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 2025-10-10.