Nenda kwa yaliyomo

Margaret Ghogha Molomo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Margaret Ghogha Molomo ni mwanaharakati wa mazingira kutoka Afrika Kusini ambaye hufanya kampeni dhidi ya maslahi ya uchimbaji madini ili kutetea haki ya mazingira bora[1]. Anatoka kijiji cha Masodi, Mokopane katika Mkoa wa Limpopo nchini Afrika Kusini.[2]

Uanaharakati wa mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Molomo ni mwenyekiti wa mtandao wa jumuiya ya Haki za Madini na Mazingira nchini Afrika kusini (MEJCON-SA) na mratibu wa shirika lake la kijamii, liitwalo The Kopano Formation Committee.[3] MEJCON-SA ni shirika linaloratibu vikundi ambavyo haki zake zimeathiriwa na shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo,[4] linalofanya kazi tangu mwaka 2012.[5]

Molomo aliisaidia jamii ya Mokopane katika mgogoro na kampuni ya uchimbaji madini ya platinam ambayo ilijaribu kufanya kazi katika ardhi inayotumiwa na jamii ya Mokopane, Limpopo, bila idhini yao. Zaidi ya hayo, mgodi huo ulikuwa ukiendesha shughuli za uchimbaji madini katika ardhi iliyotengwa kwa madhumuni ya kilimo na katika maeneo ambayo yalikuwa na baadhi ya makaburi ya jamii. Molomo na MEJCON walitaka kulinda haki za jamii kwa kuwasilisha rufaa za kisheria na kufanya michakato ya mahakama.

Wakati wa janga la COVID-19, kazi ya Molomo ilizidi kuwa ngumu kutokana na kutoweza kukusanyika kuandamana na ukosefu wa miundombinu ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini nchini Afrika Kusini, amefanya kazi ya kuongeza uelewa kuhusu desturi na majukumu ya wanawake katika vijiji vya Limpopo, ambavyo vingi vimezidi kuwa na hali ngumu na Uwezo hafifu kutokana na janga hilo la COVID-19. Pia amekuw na wasiwasi kwamba makampuni ya madini yanaweza kutumia fursa ya kutokuweza kwa wanakijiji kutekeleza haki zao za kitamaduni kwa kuingilia zaidi ardhi za mababu na maeneo muhimu ya kitamaduni.

  1. "@UN Human Rights Southern Africa on Twitter", Twitter (kwa Kijerumani), iliwekwa mnamo 2025-11-15
  2. "South African environmental activist demands responsible business practices during COVID-19". OHCHR (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-11-15.
  3. "Mining and Environmental Justice Community Network of South Africa". Centre for Environmental Rights (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-11-15.
  4. "About". MEJCON-SA (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-11-15.
  5. https://www.ohchr.org/sites/default/files/Documents/Issues/Women/WRGS/DefendingRightsinthetimeofCovid-19.pdf