Margaret Busby
| Margaret Busby | |
Busby February 2019 | |
| Amezaliwa | 1944 Accra, Gold Coast (koloni ya British ) |
|---|---|
| Majina mengine | Nana Akua Ackon |
Margaret Yvonne Busby (pia anajulikana kwa jina la Nana Akua Ackon; alizaliwa mwaka 1944) ni mchapishaji, mhariri, mwandishi, na mtangazaji mwenye asili ya Ghana anayeishi Uingereza.[1][2].
Alikuwa mchapishaji mwenye umri mdogo zaidi nchini Uingereza, na pia mwanamke wa kwanza Mweusi kuwa mchapishaji wa vitabu nchini Uingereza, wakati yeye pamoja na Clive Allison (1944–2011) walipoanzisha kampuni ya uchapishaji yenye makao yake London, iitwayo Allison and Busby (A & B), katika miaka ya 1960. Alihariri mkusanyiko wa hadithi uitwao Daughters of Africa (1992), na toleo lake la kufuatia la mwaka 2019 lililoitwa New Daughters of Africa.[3][4]
Ni mshindi wa Tuzo ya Benson kutoka Royal Society of Literature.Mnamo mwaka 2020, alichaguliwa kuwa miongoni mwa watu 100 Waingereza Weusi Mashuhuri (100 Great Black Britons).Mwaka 2021, alitunukiwa Tuzo ya Mafanikio ya Maisha Nzima (Lifetime Achievement Award) kutoka London Book Fair.Na mwaka 2023, Margaret Busby aliteuliwa kuwa rais wa English PEN, shirika linalotetea uhuru wa kujieleza kwa waandishi duniani.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "African Writing Online; Profiles; African-British Writing in Britain; The List". www.african-writing.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-05-21. Iliwekwa mnamo 2025-08-19.
- ↑ "Margaret Busby". Myriad (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-06-26. Iliwekwa mnamo 2025-08-19.
- ↑ Busby, Margaret (2011-08-03), "Clive Allison obituary", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2025-08-19
- ↑ "Black History Month in Britain: Great women you should know about", BBC Newsround (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2017-10-01, iliwekwa mnamo 2025-08-19
| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Margaret Busby kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |