Nenda kwa yaliyomo

Marehemu wote

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Marehemu Wote)
Siku ya marehemu wote, mchoro wa Jakub Schikaneder, 1888.

Marehemu wote ni adhimisho la baadhi ya madhehebu ya Ukristo kulingana na imani katika hali ya watu waliofariki dunia. Kwa baadhi yake ni suala la kuwakumbuka tu, kwa baadhi ni suala la kuwaombea pia [1].

Ni muhimu hasa katika Kanisa la Kilatini (ambalo linaliadhimisha tarehe 2 Novemba[2], mara baada ya sherehe ya Watakatifu wote) na katika Ukristo wa mashariki (ambao linaliadhimisha mara kadhaa kwa mwaka, hasa kila Jumamosi, ambayo ndiyo siku ya Yesu kukaa kaburini kabla hajafufuka Siku ya Bwana).

Katika madhehebu hayo Kanisa, kama vile linashangilia kwa sifa za kufaa wanae wote wanaoshiriki tayari heri ya mbinguni, linawajibika pia kuziombea kwa Mungu roho za wale wote ambao walitangulia kuishi kadiri ya imani wakalala wakitumaini ufufuko na za wale wote ambao, tangu ulimwengu kuumbwa, Mungu tu alijua imani yao, ili kwa kutakaswa madoa yote ya dhambi, waingie ushirika wa mbinguni na kufurahia kumuona Mwenyezi Mungu alivyo [3].

  1. Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 84
  2. Martyrologium Romanum
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/20550

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 402-405
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 386-387
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 339-341

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marehemu wote kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.