Nenda kwa yaliyomo

Marco Antonio Colonna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Marco Antonio Colonna (15231597) alikuwa askofu na kardinali wa Kanisa Katoliki.[1]

Akiwa mwanachama wa familia ya Colonna, Marco Antonio alizaliwa mjini Roma mnamo 1523, akiwa mtoto wa wakuu wa Roma, Camillo Colonna na Vittoria Colonna. Alikuwa mtoto wa ndugu wa Kardinali Pompeo Colonna. Alisomea falsafa na teolojia ya Kikristo chini ya Felice Peretti, ambaye baadaye alichaguliwa kuwa Papa Sixtus V mnamo 1585.

  1. Miranda, Salvador. "COLONNA, seniore, Marco Antonio (1523-1597)". The Cardinals of the Holy Roman Church. Florida International University. OCLC 53276621. Iliwekwa mnamo 29 Februari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.