Marcelle de Manziarly
Mandhari
Marcelle de Manziarly (13 Oktoba 1899 – 12 Mei 1989) alikuwa mpiga piano, mwalimu wa muziki, kondakta na mtunzi wa muziki wa Kifaransa.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa tarehe 13 Oktoba 1899 katika Kharkiv, na alisoma muziki mjini Paris chini ya Nadia Boulanger. Akiwa na umri wa miaka 23 tayari alikuwa ametunga kazi mbili za muziki zilizokomaa.
Baadaye alisomea uongozaji wa muziki (conducting) chini ya Felix Weingartner huko Basel, na masomo ya piano chini ya Isabelle Vengerova katika New York City. Alifundisha na kutumbuiza muziki katika Ulaya na Marekani.
Mtunzi wa muziki Aaron Copland alimwekea wakfu wimbo wake “Heart, We Will Forget Him”.[1][2]
Alifariki katika Ojai, California akiwa na umri wa miaka 89.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Riley, Matthew (2010). British Music and Modernism, 1895-1960.
- ↑ Dees, Pamela Youngdahl (2004). A Guide to Piano Music by Women Composers: Women born after 1900.
- ↑ Sadie, Julie Anne; Samuel, Rhian (1994). The Norton/Grove dictionary of women composers.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Marcelle de Manziarly kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |