Nenda kwa yaliyomo

Marcella Liburd

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marcella Liburd

Dame Marcella Althea Liburd (alizaliwa Julai 1953)[1] ni mwanasiasa kutoka Saint Kitts na Nevis.Yeye ni gavana mkuu wa tano wa Saint Kitts na Nevis tangu 2023. Alipata mafunzo ya ualimu na kisha akasomea sheria na kuwa wakili. Liburd alikuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu kama spika wa bunge la kitaifa la Saint Kitts na Nevis  wakati huo huo akiwa gavana mkuu, na pia alikuwa  gavana mkuu wa kwanza kuteuliwa na mfalme Charles III (badala ya kuhamishwa kutoka utawala wa malkia Elizabeth II). Amehudumu katika nyadhifa mbalimbali za uwaziri ikiwa ni pamoja na kaimu waziri mkuu na mwenyekiti wa upinzani wa Chama cha Labour. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu kama mwenyekiti katika historia ya shirika hilo lenye umri wa miaka 81.

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Marcella Liburd alizaliwa Julai, 1953 katika eneo la Basseterre, Saint Kitts na Nevis[2] kwa Anne Eliza na Clement Liburd.[3] Baada ya kusoma shule ya wasichana , ndipo alihitimu shule ya elimu ya sekondari ya Basseterre. Yeye alipata Shahada ya Awali ya Sanaa katika Chuo Kikuu cha West Indies mwaka 1976.[2]

Liburd alirudi kutoka nje ya nchi na kuanza kufundisha katika Shule za sekondari za Basseterre na Cayon. Alirudi kusoma  katika Shule ya Sheria ya Norman Manley ambapo alipata Shahada ya Awali ya Sheria kwa heshima mwaka 1992, alipata Cheti cha Elimu ya Kisheria mwaka 1994. Baada ya Liburd kusajiliwa kama wakili wa mahakama kuu ya mashariki mwaka 1994, alianza kazi ya kisiasa. Aliteuliwa kuwa Katibu wa Chama cha Labour mwaka 1997. Mnamo mwaka 2004, akawa spika wa bunge la kitaifa,[2] kuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo nchini.[4] Liburd alihudumu hadi mwaka 2008, alipogombea kama mgombea wa jimbo nambari 2, St. Kitts na akachaguliwa kuwa mbunge.[2]

Mnamo mwaka 2013, Liburd akawa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Labour katika historia yake ya miaka 81.[5] Mnamo mwaka 2015, Chama cha Labour kiliondolewa ofisini kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka ishirini, na kumfanya kuwa mwanachama wa upinzani.[6] Alikuwa naibu kiongozi wa kwanza mwanamke wa Chama cha Labour mwaka 2018 na akateuliwa kuwa Naibu wa Gavana Mkuu mwaka 2022. Liburd aliwekwa kama mwanamke wa kwanza kuwa Gavana Mkuu wa Shirikisho la St Kitts na Nevis mnamo februari 2023.[7] Baadaye wiki hiyo, aliteuliwa kuwa Dame Grand Cross kwa Amri ya Mtakatifu Michael and Mtakatifu George.[8][9]

  1. "Hon. Marcella Liburd – St. Kitts-Nevis Labour Party". www.stkittsnevislabourparty.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  2. 1 2 3 4 "Caribbean Elections | St. Kitts and Nevis Elections 2009". caribbeanelections.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-09-20. Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  3. "Historic Basseterre". historicbasseterre.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-26. Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  4. disseminateit@gmail.com. "St. Kitts News - Labour Spokesman: Marcella Liburd: ¡°Politics is about developing people¡± By Lesroy W.Williams". www.labourspokesman.com. Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  5. Toni Frederick. "Liburd: No Confidence Motion not discussed at Labour Conference". WINN FM 98.9 (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-07-18. Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  6. ""We Welcome The Investigations" Says MP Liburd", Antigua Observer Newspaper (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2016-02-18, iliwekwa mnamo 2026-01-31
  7. "HER EXCELLENCY MARCELLA LIBURD JP SWORN IN AS ST. KITTS AND NEVIS' FIRST FEMALE GOVERNOR-GENERAL". SKNIS (kwa American English). 2023-02-01. Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  8. "SKNVibes | Her Excellency Dame Marcella Liburd GCMG, JP installed as the first female Governor-General of St. Christopher and Nevis". www.sknvibes.com. Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  9. "The London Gazette", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2026-01-24, iliwekwa mnamo 2026-01-31