Nenda kwa yaliyomo

Marc Andreessen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Marc Andreessen (Alizaliwa 9 Julai, 1971) ni mfanyabiashara, mwekezaji wa mtaji wa hatari (venture capitalist), na mhandisi wa zamani wa programu nchini Marekani. Alijulikana kwa kuwa mwanzilishi mwenza wa Netscape na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya uwekezaji Andreessen Horowitz (a16z).[1] Alikuwa mwandishi mwenza wa Mosaic, kivinjari cha kwanza cha wavuti kuonyesha picha.[2] Pia alianzisha na kuuza kampuni ya Opsware kwa Hewlett-Packard.[3] Mnamo Januari 2025, utajiri wake ulikadiriwa kuwa dola bilioni 1.9.[4] Aliteuliwa na Rais Donald Trump kuwa mshauri katika Baraza la Wasaidizi wa Sayansi na Teknolojia (PCAST) mwaka 2026.[5]

  1. Simone Payment, Marc Andreessen and Jim Clark: The Founders of Netscape, The Rosen Publishing Group, 2006, p. 15.
  2. Calore, Michael. "April 22, 1993: Mosaic Browser Lights Up Web With Color, Creativity". Wired.
  3. Martens, China. "HP Buying Opsware in $1.6 Billion Deal". PC World.
  4. "Marc Andreessen". Forbes.
  5. "President Trump Announces Appointments to President's Council of Advisors on Science and Technology". The White House. March 25, 2026.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marc Andreessen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.