Maporomoko ya Wli
Maporomoko ya Wli ndiyo maporomoko ya maji marefu zaidi nchini Ghana na pia yanachukuliwa kuwa marefu zaidi Afrika Magharibi.[1]
Maporomoko haya yana sehemu mbili: maporomoko ya juu na ya chini.
Mahali
[hariri | hariri chanzo]Maporomoko ya Wli yapo takribani kilomita 20 kutoka mji wa Hohoe katika Mkoa wa Volta nchini Ghana, na yapo umbali wa takribani kilomita 280 kutoka mji mkuu Accra.[2]
Mazingira ya asili
[hariri | hariri chanzo]Eneo la maporomoko haya liko ndani ya hifadhi ya wanyamapori ya Agumatsa, ambayo ina misitu yenye viumbe mbalimbali. Wageni wanaweza kuona popo wa matunda, vipepeo, ndege, nyani na pia sokwe.[3]
Pia kuna koloni kubwa la popo wanaoishi kwenye miamba na kuruka angani karibu na maporomoko hayo.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Maporomoko ya Wli yanajulikana pia kwa jina la wenyeji “Agoomatsa”, likimaanisha “Niruhusu nitiririke.” Inasemekana yaligunduliwa na kundi la wawindaji waliodhani sauti ya maji ilikuwa ngoma ya kuzungumza (talking drum), wakaifuata hadi wakagundua kuwa ilikuwa ni maporomoko ya maji.
Maporomoko haya yako katika eneo la utamaduni wa Waewe (Ewe culture) na ni moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini Ghana.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Wli Waterfall: A Tourist Attraction Worth Visiting". Modern Ghana (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-06-18.
- ↑ "Page Not Found - Easy Track Ghana". www.easytrackghana.com. Iliwekwa mnamo 2026-06-18.
{{cite web}}: Cite uses generic title (help) - ↑ "Wli waterfalls in Ghana". independent-travellers.com. Iliwekwa mnamo 2026-06-18.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ghana bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Maporomoko ya Wli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |