Nenda kwa yaliyomo

Maporomoko ya Boyoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maporomoko ya Boyoma

Maporomoko ya Boyoma ni ufuatano wa maporomoko saba ya mto Kongo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwenye maporomoko haya yanayoenea kwa kilomita 100 hivi mto unashuka mita 61[1].

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Maporomoko ya Boyoma hutazamiwa kuwa mpaka baina mto Kongo mwenyewe na sehemu yake inayoitwa Lualaba. Hayapitiki na meli au boti kwa hiyo kuna reli ndogo inayobeba mizigo kati ya miji ya Ubundu und Kisangani.

Ilhali mto Lualaba (jinsi sehemu kubwa ya kwanza ya mto Kongo huitwa) una mwendo wa kuelekea kaskazini, ndani ya maporomoko ya Boyoma huanza pinde kubwa linalopeleka mto kuelekea magharibz.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Kwa muda mrefu maporomoko yalijulikana kwa jina la "Stanley Falls" kutokana na mpelelezi Henry Morton Stanley aliyekuwa mtu wa kwanza wa kupeleka maelezo yake kwa umma wa kitaalamu ya kimataifa[2]. Aliunda pia ktuo cha kwanza kwenye mwisho wa maporomoka kilichoendele mji wa Stanleyville unaoitwa Kisangani tangu mwaka 1966.

Ilhali jina la eneo la Stanleyville iliitwa zamani "Boyoma" basi maporonoko yalikopkea jina hili.

Viungo vya Nje na Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Boyoma Falls, Encyclopedia Britannica
  • Stanley, H.M., 1899, Through the Dark Continent, London: G. Newnes, Vol. Two, uk. 223 ff (chapter VIII), inapatikana mtandanoni kwa archive.org