Nenda kwa yaliyomo

Shirika la Roho Mtakatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mapadri wa Roho Mtakatifu)
Muhuri wa shirika ukionyesha Moyo Safi wa Maria, na Roho Mtakatifu akitokea katika Utatu Mtakatifu.

Shirika la Roho Mtakatifu (kwa Kiingereza: Congregation of the Holy Spirit under the protection of the Immaculate Heart of the Virgin Mary; kwa Kilatini: Congregatio Sancti Spiritus sub tutela Immaculati Cordis Beatissimae Virginis Mariae) ni shirika la kitawa la kimisionari liliongoza kwa muda mrefu kati ya mashirika yote ya Kanisa Katoliki yaliyofanya kazi hiyo. Ndio waliolianzisha nchini Tanzania na sehemu nyingine nyingi hasa za Afrika. Wanashirika wanaitwa mara nyingi Waspiritani na hutumia kifupisho CSSp.[1]

Huko Roma, tarehe 29 Aprili 1979, Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri Jacques-Désiré Laval (18 Septemba 1803 – 9 Septemba 1864), padri anayeitwa "Mtume wa Morisi", aliyepata hivyo kuwa mwanashirika wa kwanza kupewa heshima hiyo.[2], akifuatwa na Daniel Jules Alexis Brottier (7 Septemba 1876 – 28 Februari 1936), padri na mmisionari huko Senegal, aliyetangazwa na Papa huyohuyo tarehe 25 Novemba 1984.

Mwaka 2018 Waspiritani walikuwa 2,794 karibu duniani kote (wakiwemo mapadri 2,109) [3].

  1. "Spiritans.org". The Congregation of the Holy Spirit Province of the United States.
  2. "Jacques Désiré Laval", Dictionary of African Christian Biography
  3. "Congregation of the Holy Spirit (C.S.Sp.)". www.gcatholic.org.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shirika la Roho Mtakatifu kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.