Rangi ya manjano
Mandhari
(Elekezwa kutoka Manjano (rangi))
Rangi ya manjano, manjano kwa kifupi au njano ni rangi inayofanana na ile ya unga wa manjano. Ni rangi ya matunda mabivu kadhaa, kama vile chungwa (aina njano), papai, embe, ndizi n.k.
Ni mojawapo ya rangi zitumikazo kwa kazi mbalimbali kama katika kuchora michoro mbalimbali na kadhalika.
Michoro hiyo inaweza kuwa ya kitu chochote kama vile: wanyama, wadudu, watu, mimea na hata vitu visivyo na uhai kama vile mawe, majengo n.k.
Hivi vyote katika kuvichora unaweza kutumia rangi mbalimbali kama rangi ya njano, kijani, nyekundu, bluu, zambarau, kahawia na rangi nyinginezo.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |