Mandakini (muigizaji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mandakini (muigizaji)
Mandakini mnamo Desemba 2012
Mandakini mnamo Desemba 2012

Mandakini Kihindi: मंदाकिनी Kigezo:IPA2 ITRANS: Mandakini) (alizaliwa 7 Januari 1969, kama Yasmeen Yusuf) ni mwigizaji wa zamani wa Bollywood. Kazi ilikuwa ya muda mfupi, lakini yenye utata katika vipindi za Kihindi na ilisemekana kuwa ana uhusiano na mwanaharamu Dawood Ibrahim. [1]

Maisha Yake ya Utotoni[hariri | hariri chanzo]

Mandakini alizaliwa katika familia ya Anglo Indian katika Meerut mama yake ni Mhindu na baba yake ni Muingereza.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Wasifu wa Awali[hariri | hariri chanzo]

Akiwa na miaka 16,alipewa jukumu kuu katika sinema zaRaj Kapoor mwaka wa 1985 , Ram Teri ganga Maili kinyume cha mwana wake mdogo, Rajiv Kapoor. Sinema hiyo ilivuma, na kufanya Mandakini kuteuliwa katika tuzoFilmfare kama muigizaji mwanamke bora.[2]. Filamu lilisabisha zogo kwa sababu ya sehemu mbili - moja ambayo Mandakini anaoga katika mto amevaa nguo nyeupe ambayo matiti yake yalikuwa yakionekana wazi, na sehemu nyingine alionyeshwa akinyonyesha mtoto. Baadhi ya wakosoaji walidai kwamba zilikuwz za kuudhi na aibu, na zilienda kinyume cha masharti Bodi ya India ya Filamu ambazo hazikukubali Uchi. Kapoor, kama kawaida,alitetea kuingizwa kwa sehemu hizi akisema zilikuwa za kupendeza.

Mandakini aliweza kuiiza katika filamu chache zilizofanikiwa, kama Dance Dance, pamoja na Mithun Chakraborty Karke Pyaar Dekho na Govinda, lakini kamwe hakuweza kutengeneza mafanikio ya sinema yake ya kwanza.

Uhusiano na Dawood[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka 1994, picha zilianza kuzungushwa ambapo Mandakini akiwa na mkora hatari Dawood Ibrahim. Uvumi ulikuwa tayari unazunguka kwamba walikuwa kitu kimoja. Moja ya nadharia zilizokuweko ni kuwa Ibrahim, ambaye alikuwa anajulikana kuwa na nia riba katika Bollywood na kusadia filamu kadhaa kwa fedha, alimkaba Rishi Kapoor kushirikisha Mandakini katika filamu, na kwa kweli alikuwa bibi yake. Baadaye iliripotiwa kwamba alikuwa hata amehamia Dubaiili kuwa pamoja naye.[1]

Mandakini alikanusha uvumi kuwa alikuwa pamoja na Dawood. Wakati yeye alikubali kama marafiki , alidai kwamba hawakujuana binafsi, sembuse kuwa wanandoa.[3] Pia alisema kuwa yeye alikuwa ameolewa na R. Thakur, daktari katika Mumbai, na hata kuzaa mwana wa mume mwaka wa 1995.

Hata hivyo, uvumi kamwe ulikoma. Nadharia mmoja iliyodai kwamba kuwa Mandakini na Dawood, lakini na ndugu yake Abbas, ambaye alimoa kwa siri. Ilisemekana kwamba alikuwa na mwana kutoka kwa mmoja wa ndugu ambaye alilelewa USA.[1]

Maandishi ya italiki===Kazi ya hivi karibuni=== Wasifu wa mandakini ulikwabwa na msingi mbaya. Alijiuzulu baada yaZordaar mwaka wa 1996, na ameishi katika Mumbai pamoja na mumewe na mwana. Tangu hapo, amejaribu kujiunda tena mwenyewe. Alitoa albamu mbili za nyimbo za pop No Vacancy na Shambala -lakini hakuna yeyote iliyofanikiwa. Hivi sasa, yeye anaendesha madarasa ya Tibetyoga na ni mfuasi wa Dalai Lama.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 Gangadhar, V. "The price of fortune", The Hindu, N. Ram, 2002-11-01. Retrieved on 2008-09-15. Archived from the original on 2011-07-26. 
  2. Filmfare Awards (PDF) 71. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-06-12. Iliwekwa mnamo 2008-09-14.
  3. Walia, Nona. "Mandakini: ‘I know Dawood but I’m not his woman’", Indiatimes Movies, Times of India, 2005-02-25. Retrieved on 2008-09-15. Archived from the original on 2009-02-01.