Nenda kwa yaliyomo

Mame Diarra Bousso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mame Diarra Bousso (1833 - 1866) alizaliwa na Serigne Mouhamadou Bousso na Sokhna Asta Wâlo Mbackein katika mwaka wa 1833 huko Mbusôbé, mji wa kaskazini-mashariki mwa Senegal siku hizi unaohusishwa na Podor.

Alifariki akiwa na umri mdogo wa miaka 33 mwaka wa 1866 na alizikwa Porokhane.

Urithi na utakatifu

[hariri | hariri chanzo]

Hadi leo hii, maelfu ya watu husafiri kwenda kuhiji kila mwaka hadi mahali alipofariki na kwenye kaburi lake huko Porokhane, Senegal, hija pekee ya Kiislamu iliyotengwa kwa ajili ya mwanamke nchini Senegal. Eneo hilo pia linajumuisha msikiti pamoja na eneo la ufundi kwa ajili ya mtoto wa kike kupata elimu na mafunzo.

Bousso pia huadhimishwa siku ya kufarikikwake katika ugenini wa Waafrika miongoni mwa baadhi ya jamii za wahamiaji. Huko Harlem, wanaume pamoja na wanawake hukusanyika kusimulia kile wanachoamini kuwa miujiza yake, na watoto wake Amadou Bamba, anasoma mashairi yake, na pia huwasikiliza wanamuziki wakiimba kuhusu maisha yake. [1]

Usomaji zaidi

[hariri | hariri chanzo]
  1. Abdullah, Zain (2010-09-01). Black Mecca: The African Muslims of Harlem (kwa Kiingereza). Oxford University Press. ISBN 9780199813612.