Makumbusho ya kutokutambua uovu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makumbusho ya kutokutambua uovu (kwa Kituruki Masumiyet Müzesi) ni riwaya iliyoandikwa na Orhan Pamuk na kutolewa mwaka wa 2008.

Maelezo kutoka redio ya Kituruki[hariri | hariri chanzo]

Katika fasihi ya Kituruki, waandishi wa mashairi mbalimbali wametumia muda wao kutaja sifa na uzuri wa jiji la Istanbul. Kuna waaandishi wengi wa vitabu vya historia, mapenzi na hadithi mbalimbal ambao pia hawakusita kuusifia mji huu wa kimataifa. Lakini uzuri wa mji huu si tu kwa muonekano bali hata vitabu na mashairi yameshindwa kusifia kiwango ambacho kinatakiwa. Istanbul ni mji wa upendo, na mashairi mengi yanaelezea mapenzi ya watu maarufu ambao waliishi Istanbul katika kipindi cha nyuma. Leo hii tutakuhadithia simulizi ya mtu ambaye alitengeneza sehemu ya makumbusho ya upendo. Upendo huu umeelezewa ndani ya riwaya. Lakini kujua kwamba riwaya hii imeandika historia ya kweli au ya kufikirika, tutajua mwishoni mwa kipindi chetu na wewe msikilizaji ndiye utakayetoa maamuzi. Riwaya hii iliandikwa na mwandishi wa Kituruki, Orhan Pamuk ambaye ni mshindi wa tuzo ya Nobel. Riwaya hii ni maarufu kama ulivyo maarufu mji wa Istanbul wenyewe na ni riwaya ambayo haitokuja kusahaulika. Riwaya hii ni moja ya vitu vilivyomletea Pamuk tuzo hii ya Nobel. Riwaya yake iliyopewa jina la Istanbul, imeelezea maisha halisi ndani ya jiji hili. Riwaya hii ilipelekea kupatikana kwa tuzo ya Nobel Prize ambayo Pamuk aliitwaa. Sasa tuanze kukupa historia yenyewe. Kama tulivyosema hapo awali leo hii riwaya yetu inazungumzia jumba la makumbusho ya upendo. kijana mwenye umri wa miaka 30, Kemal ambaye anatokea katika familia tajiri ya Basmaci ambayo inamiliki viwanda vya nguo anampenda Fusun, binti mwenye umri wa miaka 18 ambaye anatokea katika familia ya kimaskini. Mwandishi wa riwaya hii ya kuvutia ya mapenzi anagusia maisha halisi katka mitaa ya Istanbul na majarida ya udaku ambayo ni mashuhuri ndani ya mji huu. Historia hii ya mapenzi ambayo yameanza tangu mwaka 1975 baina ya Kemal na Fusun na kudumu mpaka sasa, inaelezewa ndani ya riwaya hii ya “museum of innocence”. Kwa wale ambao hawakubahatika kuisoma riwaya hii. Jina hili la “museum of innocence” sio tu ni jina la riwaya, bali ni jina la jumba la makumbusho ambalo kwa muda mrefu, Orhan Pamuk alilifikiria. Uziinduzi wa jumba hili la makumbusho ni sehemu ya riwaya hii. Kabla ya kuanza kuandika riwaya hii katika miaka ya 70 na 80, Pamuk alifanya kazi ya ununuzi wa vitu ambavyo vilitumiwa na waandishi mashuhuri wa riwaya wa kipindi hicho. Alikusanya pia vitu vyote ambavyo aliviandika ndani ya riwaya hii. Pamuk alikua akifanya vitu viwilii kwa wakati mmoja, yaani huku anaandika riwaya na kwa upande mwingine anaandaa jumba hili la makumbusho. Jumba hili lilitarajiwa kuwekwa vitu ambavyo mhusika mkuu wa riwaya hii, Kemal na mpenzi wake Fusun watavtumia. Kwasababu riwaya hii inamuelezea shujaa wa mapenzi , Kemal kuwa alikusanya vitu vyote ambavyo mpenzi wake Fusun alivitumia na kuvihifadhi sehemu moja. Jumba hili lina viatu vya rangi ya njano pamoja na heleni ambazo Fusun alizitumia kuanzia mwanzo hadi mwisho wa riwaya hii.

Kama ilivyo katika riwaya, ambapo Kemal aliamua kufungua jumba la makumbusho kwa kuweka vitu vya Fusun, naye muandishi Pamuk akaona ni vema atengeneze sehemu ya makumbusho. Alilifanyia matengenezo jengo lake la Çukurcuma alilolinunua miaka mingi nyuma kwa ajili ya kukamilisha ndoto hii. Mradi huu wa kuanzisha sehemu ya makumbusho inayohusiana na riwaya, uliungwa mkono na kitengo cha makao makuu ya utamaduni wa Ulaya 2010. Jengo hili lilifunguliwa mnamo mwezi Agosti mwaka 2010. Baada ya kukamilika kwa ssehemu hiyo ya makumbusho, Orhan alikusanya vitu vyote vya ukumbusho wa utamaduni wa Istanbul tangu mwaka 1950 hadi mwaka 2000. Matengenezo yake yalifanywa na wabunifu wa Kijerumani, Brigite na Gregor Sunder Plassman. Na hapa tumefikia mwisho wa kipindi cha leo.