Maksimo Muungamadini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha ya Mt. Maksimo kadiri ya mtindo wa Ukristo wa mashariki.

Maksimo Muungamadini alizaliwa mwaka 580 akafariki Schemaris (Lazica) mwaka 662.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na wengineo kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 21 Januari au 13 Agosti.

Jina la pili aliongezewa kutokana na mateso yaliyompata kwa ajili ya imani sahihi: alikatwa mkono wa kulia na ulimi asiweze kuendelea kuitetea wala kwa maandishi wala kwa sauti.

Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli ulimpa ushindi baada ya kifo chake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Vita ac certamen S. Maximi (PL 90,67-110): Wasifu rasmi kwa Kilatini.
  • P. Sherwood, St Maximus the Confessor. London, 1955
  • Jean-Claude Larchet, Saint Maxime Le Confesseur. Paris, 2003

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]