Makena Onjerika

Makena Onjerika (alizaliwa miaka ya 1980) ni mwandishi mwenye asili ya Kenya, ambaye alishinda Cain prize for African printing ya mwaka wa 2018[1], na kumfanya kuwa mwandishi wa nne kutoka nchi yake kulinyakua taji hilo-kufuatia ushindi wa Binyavanga Wainaina mwaka wa 2002 na Yvonne Adhiambo Owuor mwaka wa 2003 na Okwiri Oduor mwaka wa 2013[2].
Mnamo Julai mwaka wa 2018, Makena alishinda Tuzo ya Caine prize for african writing[3] - ambayo mara nyingi hufasiriwa kama tuzo kuu ya fasihi barani Afrika, kwa hadithi yake fupi yenye mada "Fanta Blackcurrant", iliyochapishwa katika jarida la Wasafiri la mwaka wa (2017). Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi wa Tuzo ya Caine Prize, mwandishi na msimulizi mashuhuri na mshindi wa tuzo mMarekani mwenye asili ya Ethiopia Dinaw Mengestu, alimtangaza Makena kama mshindi wa zawadi ya £10,000 katika hafla ya chakula cha jioni ya utoaji tuzo.[4] Sherehe ilifanyika kwa mara ya pili mtawalia katika Baraza la Seneti la Chuo Kikuu cha London, kwa ushirikiano na SOAS na Kituo cha Mafunzo cha African studies. Mengestu alisifu hadithi hiyo katika matamshi yake, akisema: "...mshindi wa Tuzo ya Caine prize ya mwaka huu ni mwenye ushupavu wa kipekee - simulizi la kiubunfu lakini lisilofafanuliwa na mitaa ya Nairobi, hadithi ambayo inajikita kama zaidi ya shahidi. 'Fanta Blackcurrant' ya Makena Onjerika inadhibiti sarufi na uundaji wa muundo wakipekee ulio undwa nayo yenyewe, na inakwepa hali yoyote ya uhisia wa kimapenzi kwa manufaa ya simulizi linalotia kiwewe kupitia ucheshi na huzuni."[5]
Makena ni mhitimu wa programu ya Uandishi wa Ubunifu wa MFA katika Chuo Kikuu cha New York , na imechapishwa katika Urban Confusions na Wasafiri . Anaishi Nairobi, Kenya, na kwa sasa anatayarisha riwaya ya njozi. Yeye ni mchangiaji wa anthologia ya 2019 ya New Daughters of Africa, iliyohaririwa na Margaret Busby.[6]
Makena alianzisha Warsha ya Kuandika Fiction Nairobi na kuhariri anthologia ya Digital Bedbugs, iliyojumuisha hadithi kutoka kwenye warsha hiyo. [7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The Winner — The Caine Prize for African Writing". The Caine Prize for African Writing (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-12. Iliwekwa mnamo 2025-10-08.
- ↑ "Makena Onjerika Awarded 2018 Caine Prize, Is 4th Kenyan Winner". Brittle Paper (kwa American English). 2018-07-02. Iliwekwa mnamo 2025-10-08.
- ↑ "Kenyan Makena Onjerika wins 2018 Caine Prize for African Writing". Daily Nation (kwa Kiingereza). 2020-07-02. Iliwekwa mnamo 2025-10-08.
- ↑ "The Star". The Star (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-18. Iliwekwa mnamo 2025-10-08.
- ↑ "Kenya: 2018 Winner - Makena Onjerika (Kenya)", allAfrica.com (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2025-10-08
- ↑ Daughters of Africa | Contents" (PDF). Myriad Editions. pp. vii–xiv. Retrieved 5 March 2024.
- ↑ Murua, James (2020-02-18). "Makena Onjerika-edited anthology 'Digital Bedbugs' available for your reading pleasure". Writing Africa (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-05-11.