Orodha ya makabila ya Kenya


Hii orodha ya makabila ya Kenya inatokana na orodha ya lugha za Kenya iliyotolewa na Ethnologue.
Ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Kenya, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Kenya na nchi za jirani.
Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi Kenya kama wakimbizi kutoka vita katika nchi za jirani, wala vikundi vya wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Arabia, Uhindi au nchi nyinginezo.
Kenya ina lugha rasmi Kiingereza na Kiswahili, lakini kuna zaidi ya lugha 60 za asili zinazotumika katika maisha ya kila siku.[1][2][3]
Makabila makuu
[hariri | hariri chanzo]Makabila ya Kenya ni zaidi ya 40, kila moja ikiwa na tamaduni na lugha za kipekee na yakigawanyika katika makundi makuu ya lugha: Wabantu, Waniloti, na Wakushi. Asilimia inaonyesha mgao wao ukifananishwa na idadi yote ya Wakenya[4]:
- Wakikuyu (Agĩkũyũ) 17.13% – kundi kubwa zaidi, wanaishi maeneo ya kati, huzungumza Kikuyu, wanajulikana kwa kilimo na biashara.
- Waluhya 14.35% – jamii ya magharibi, huzungumza lahaja mbalimbali za Kiluhya, wanajulikana kwa tamaduni za muziki na sherehe.
- Wakalenjin 13.37% – jamii ya Bonde la Ufa, huzungumza lahaja za Kalenjin, wanajulikana kwa utamaduni wa wanariadha.
- Wajaluo 10.65% – jamii ya Ziwa Viktoria, huzungumza Dholuo, wanajulikana kwa uvuvi na tamaduni za muziki.
- Wakamba 9.81% – jamii ya mashariki, huzungumza Kikamba, wanajulikana kwa ususi na biashara ya mitumba.
- Wasomali 5.85% – jamii ya kaskazini mashariki, huzungumza Kisomali, wanajulikana kwa ufugaji na tamaduni za Kiislamu.
- Wakisii 5.68% – jamii ya nyanda za juu za kusini magharibi, huzungumza Ekegusii, wanajulikana kwa kilimo cha chai na ndizi.
- Wamijikenda 5.23%
- Wameru (Meru) 4.15%
- Wamasai
- Waturkana
- Waembu
- Wataita
- Waswahili
- Wasamburu
Makabila kwa jumla
[hariri | hariri chanzo]Kuna makabila asilia karibu arubaini nchini Kenya, yakiwemo[5]:
- Waata
- Waaweer (au Waboni)
- Wabajuni
- Waborana
- Waburji
- Wachonyi
- Wachuka
- Wadaasanach
- Wadahalo
- Wadigo
- Waduruma
- Waembu
- Waendo
- Wagikuyu
- Wagiryama
- Wagusii (au Wakisii)
- Wakalenjin (wakijumisha Wapokot, Wamarakwet, Waelgeyo, Wanandi, Wasabaot, Wakipsigis, na Watugen)
- Wakamba
- Wakore
- Wakuria
- Waluo
- Waluhya (au Waluyia, wakijumuisha Wabukusu, Wanyala, Watachoni, Wakabras, Watsotso, Waidakho, Waisukha, Wamaragoli, Wawanga, Watiriki, Wanyore, Wakhayo, Wasamia, Wakisa, Wamarama)
- Wamaasai
- Wamalakote (au Wailwana)
- Wambeere
- Wameru
- Wamijikenda
- Wamwimbi
- Waogiek (au Waokiek)
- Waorma
- Waoromo
- Wapokomo (Wapokomo wa Chini na Wapokomo wa Juu)
- Warendille
- Wasagalla
- Wasamburu
- Wasanye
- Wasengwer
- Wasomali (au Wariyaahe)
- Wasuba
- Waswahili
- Wataita
- Wataveta
- Wateso
- Watharaka
- Waturkana
- Wayaaku
Makabila mengine yasiyo ya Kenya lakini yamekaa nchini kwa miaka mingi ni:
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Ogot, B.A. (1985). Kenya: Historical and Cultural Perspectives. East African Publishing House.
- ↑ "Languages of Kenya". Ethnologue. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2025.
- ↑ Kenya Population and Housing Census 2019 (Ripoti). Kenya National Bureau of Statistics. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2025.
- ↑ "Kenya is stuck in tribalism, and calls for national unity are all too often manipulative". D+C (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-27.
- ↑ Julie Kwach (2022-03-26). "Tribes in Kenya: List and details about the Kenyan tribes". Tuko.co.ke - Kenya news. (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-27.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1989 Kenya Population Census Ilihifadhiwa 29 Novemba 2006 kwenye Wayback Machine.
- http://www.minorityrights.org/download.php?id=147 Ilihifadhiwa 14 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.