Majadiliano ya mtumiaji:Winifrida
Weka madaKaribu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
- usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
- do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
JOTO LINAPOZIDI UNAPASWA:
1. Unywe maji ya kutosha na siyo kusubiri mpaka uandikiwe na daktari. 2. Ujitahidi kuoga na siyo mpaka ushikiwe kiboko ndio ukaoge. 3. Kupunguza kunywa bia pamoja na aina nyingine za pombe hii ni kwa wale wanaotumia vinywaji hivyo. 4. Kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi na protini nyingi.
Kwa kifupi inapendeza sana ukiangalia afya yako kwa makini bila kusubiri kusukumwa na mtu na pia kuwasaidia wale wasioelewa. Kumbuka kutoa msaada kwa upendo na amani kwa sababu huo ndio utu. Boresha afya yako na ya jirani yako kipindi cha joto kali.
MWANADAMU MIMI. Mara nyingi mimi mwanadamu ninapenda kuomba msaada wa Mungu, ninapenda kuona nikitukuzwa na wengine hata kama ninafanya mambo yasiyopendeza mbele ya wenzangu na mbaya zaidi situpendi kujishusha hata pale ninapokuwa nimekosea. Vilevile ninapenda sana kumwambia Mungu anisamehe katika madhaifu yangu. Je, mara ngapi ninawafikiria wenzangu hasa walio wanyonge katika jamii yangu? Ni mara ngapi ninawapa nafasi ya kunikosoa nami kufungua moyo wangu na kupokea divai hiyo ya msaada kutoka kwa wenzangu hata kama ni chungu au chachu kiasi cha kutoupendeza moyo wangu? Je, ubabe wangu na kujikweza kwengu kuna maana yoyote kwengu binafsi na kwa wale wanaonitazama? Nawafikiria wenzangu kwa upendo wa kweli au najivika ubinafsi katika mtazamo wangu na kuwaona wengine si kitu?
Mimi mwanadamu, napaswa kuwapenda wenzangu bila ubinafsi, niwasIkilize wenzangu zaidi kuliko kuwaambia mawazo yangu kwani kujishusha kwangu kutanifkisha mbali kuliko kujikweza kwangu. Aidha napaswa kutambua kuwa safari ya kuja kwangu na kuondoka kwangu duniani ni sawa na wenzangu, hivyo basi ni vema nikajitahidi sana kuwa shahidi wa unyenyekevu na upendo kuliko kuwa mtumwa wa sifa za kijinga na majikwezo ya bure.
KIKOMBE MFANO WA MAISHA. Kila mtu anakifahamu vema kikombe, zaidi matumizi ya kikombe yanafahamika kwa kila mmoja wetu. Basi mpendwa wangu, ikiwa haufahamu matumizi ya kikombe na namna kinavyotumika katika maisha yako ya kila siku ngoja nikwambie, ni hivi kikombe hutumika katika kunywea maji, chai, uji, juisi na hata vinywaji vingine kwa sababu kwa familia nyingi hazina uwezo wa kumudu kununua bilauli za kila aina kwa kila kinywaji. Lakini kabla ya kukinywea kikombe ni lazima yafuatayo yafanyike yaani kukishika, kukiinua na kisha kukinywa kilichomo ndani yake.
Maisha yetu pia ni mfano wa kikombe kinachotakiwa kunywewa kwa kufuata utaratibu maalum yaani kushika, kuinua na kisha kunywa kilicho ndani yake. Ningependa kufafanua njia hizo tatu kama ifuatavyo:- 1.KUSHIKA KIKOMBE CHA MAISHA. Hii ni hatua ya kwanza kabisa katika safari ya maisha kwa sababu ni vigumu kukinywea kikombe bila kukishika mkononi tena kwa umakini. Kushika kikombe cha maisha ni pale ambapo mtu anajitambua yeye mwenyewe yaani kutambua vipaji na mapungufu yake na siyo kuishia hapo tu bali pia kujikubali na kujipokea mwenyewe kwanza. Ni hatua iliyo na pande mbili zisizoweza kutengana kwa sababu zinakumbatia uhalisia wa maisha ya mwanadamu. Pande hizo ni FURAHA na HUZUNI. Hatua hii ya kwanza ni muhimu sana kwa binadamu katika safari yake ya kukua. Ni hatua inayomsaidia kuwakubali na kuwapokea wengine katika hali zao mbalimbali.
2.KUINUA KIKOMBE CHA MAISHA. Hii ni hatua ya pili katika safari ya maisha. Ni hatua muhimu sana kwa sababu kamwe hauwezi kukinywea kikombe bila kukiinua. Kuinua kikombe cha maisha ni pale unaposhirikishana na ndugu, jamaa na marafiki zako furaha na huzuni zako ili kupata wigo mpana wa kutembea kwa amani. Kumbuka ukishirikisha huzuni yako kwa wenzako hupungua na ukishirikisha furaha yako kwa wenzako huongezeka na kwa kufanya hivi hujipatia BARAKA maishani. Uwazi wako wa kushirikisha maisha yako hukupatia ujasiri wa kushiriki hali za wengine katika jamii.
3.KUNYWEA KIKOMBE CHA MAISHA. Hii ni hatua ya mwisho katika safari ya maisha. Ni kunywa kilichomo ndani ya maisha yako. Wakati mwingine kinywaji chaweza kuwa kichungu sana kiasi cha kutokustahimili kukimeza lakini ni lazima kunywa kwa utaratibu na kumeza kila fundo linaloingia mdomoni. Hii ina maana kujitahidi sana kuwa mwaminifu katika misukosuko ya maisha, kutokukata tamaa hata mara moja hata ukikutana na magumu kiasi gani njiani. Ni hatua inayokusaidia kuwasaidia wenzako kwa njia ya ushuhuda wa maisha yako na siyo kwa maneno yako tu!
Yote hayo yatawezekana iwapo tu utajiweka chini ya ulinzi wa Mungu na siku zote kujitahidi kuwa mtu wa sala. Bila sala ndugu yangu kamwe hatuwezi kufanya chochote na badala yake tutajikuta tukitangatanga huku na huko bila mwelekeo wowote. Daima tumtazame Yesu kwa imani pale msalabani hasa pale tunapohisi kuwa kikombe cha maisha ni cha moto sana kukishika ama ni kizito sana kukunyanyua na kichungu mno kukinywea kwa uaminifu.
Asante sana na Mungu akubariki.
Waridi ni ua zuri sana. Ukiliangalia kwa macho linavutia sana. Lakini cha ziada ni kuwa ukiliangalia utagundua kuwa mmea wake umezungukwa na miiba lakini cha ajabu ni kuwa miiba yake kamwe haichomni ila akienda mwanadamu na kujaribu kushika bila umakini miiba humwadhibu vibaya kwa kumchoma na maumivu yake aikwambie mtu.
Sisi pia ni wazuri sana na tunapendeza mbele ya macho ya Mungu. Kila mmoja wetu ni wa pekee lakini pia kila mtu ana udhaifu wake. Lakini udhaifu huo kamwe hauondoi uzuri wetu kama ambavyo miiba haiwezi kuondoa uzuri wa waridi. Lakini tofauti ni moja tu kwamba tunashindwa kuvumiliana na kupokeana katika madhaifu yetu na ndiyo maana kila siku tunagombana ila miiba ya mawaridi inavumiliana na ndiyo maana inaishi kwa amani.
Wapendwa, tuheshimiane, tupendane na kusaidiana kwani sisi sote ni wana wa Baba Mmoja.