Majadiliano ya mtumiaji:Prince magic m
Weka madaKaribu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
- usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
- do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
--Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:49, 28 Oktoba 2020 (UTC)
RAHMA W. MAHMOUD
[hariri chanzo]Rahma W. Mahmoud (Mkenga Mbwambo) 'Maandishi ya kooze ni mwandishi wa Vitabu (Riwaya, mashairi, tamthilia) , muandaaji wa filamu na muandishi wa habari. Amezaliwa mwaka 1972, Ocean road jijini dar es salaam na kukulia katika mtaa wa Libya, kisutu (uhindini), ulipo katikati ya jiji la dar es salaam, nchini Tanzania, Afrika mashariki. Baba yake alikuwa afisa wa posta na simu na mama yake alikuwa mfanyabishara. Ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto sita. Ameolewa na Shuaybu Mahmoud Mruma. Amejaliwa kupata watoto watatu. Kabila la wazazi wake ni ni wapare wanawaotokea same, mkoani Kilimanjaro. Alipata elimu ya msingi jijini dar es salalam, akapata elimu ya sekondari mkoani Kilimanjaro. Alijiunga na chuo cha utumshi wa serikali magogoni.Baadaye alipata mafunzo mafupi ya uandishi wa habari,uwandishi wa vitabu, uchapishaji na haki miliki.
Alisomea mafunzo ya utaalamu wa nguo za wanawake katika chuo cha Sherma na ubunifu wa mitindo mbalimbali ya wanawake na watoto.
Kazi
1.Alikuwa mkurugenzi masoko thagaji investment.
2. Alifanya kazi ya uandishi wa habari business times, akiandikia gazeti la majira.
3. Alikuwa mtangazaji wa radio times fm, dar es salam Tanzania na muandaa wa vipindi vya watoto.
Mtunzi na mtayarishaji wa simulizi za mila na desturi za kumuandaa msichana katika kabila mbalimbali nchini Tanzania (mwari wetu), mapishi,utunzi wa riwaya za watu wazima katika kipindi cha siesta maisha, kupitia radio times.
Alikuwa mtangazaji na msimulizi wa sinema za kihindi katika kipindi cha nyimbo za kihindi.
Ilikuboresha vipindi vya watoto alipata mafunzo mafupi ya haki za watoto katika kuandaa na kutangaza kupitia shirika la watoto duniani (UNICEF), alishirikiana nalo katika kuandaa siku ya utangazaji za watoto duniani na siku ya mtoto wa afrika. Shughuli nyingine za jamii 1.Alikuwa mjumbe wa kamati ya maandalizi siku malaria, wizara ya afya. 2. Macmillan Aidan –Tanzania 3. Kuleana Dar es salaam 4. kihohede – dar es salaam 5. dogodogo centre 6. Child in the sun 7. Ameandika riwaya na mashairi katika magazeti ya uhuru,majira, Mwananchi, dar leo, sanifu na sport starehe
Uongozi 1. Alikuwa Katibu mwenezi wa umoja wa waandishi wa vitabu Tanzania 2. Alikuwa Katibu mkuu wa umoja wa waandishi wa vitabu wanawake Tanzania (UWAVIWATA). 3. Mjumbe wa kamati kuu ya baraza la vitabu Tanzania (BAMVITA) 1999-2001 4. Mjumbe wa kamati ya wiki ya vitabu Tanzania 1999- 2001. Uzinduzi wa vitabu Wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia na watoto, kupitia waziri, Mh: Dr. Asharose migiro walizindua vitabu vyake 14 vya watoto mwaka 2006 katika ukumbi wa wizara ya habari maelezo, jijini dar es salaam.
Chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) kupitia mkurugenzi wake Ananilea Nkya waliratibu uzinduzi huo.
Vitabu hivyo vilifadhiliwa na mashirika ya kimataifa ya SIDA, CODE na CIDA. Vinatumika katika maktaba ya shule za msingi Tanzania. Vitabu hivyo ni 1. Mwindaji kiburi- kisa cha buibui kuishi kwa binadamu 2. Malkia mroho- kisa cha mbwa akimuona chatu humfuata 3. Mateso ya mama wa kambo- Malezi mabaya ya mama wa kambo 4. Kidonda cha bahati- umuhimu wa Elimu kwa Watoto wa kabila la Kimasai na madini yaliyowazunguka. 5. Dawa ya mlafi- athari yaMtoto kula chakula kupita kiasi 6. Nani kama mama- Mapenzi ya mama kwa mtoto 7. Nangasu mtoto wa mianzini- wazazi wanaozaa na kutupa watoto wachanga. 8. Maua na chipsi dume- Ubakaji na maambukizi ya UKIMWI 9. Mawazo na adha ya usafiri- Matatizo ya usafiri kwa wanafunzi katika miji mikuu. 10. Jiwe la maafa- athari ya mila potofu za mauaji ya watoto wanaoanza kuota meno ya juu 11. Elimu ni ufunguo wa maisha- Athari ya mtoto asiyepata elimu 12. Safari tano za kadogoo- Umuhimu wa familia kusafiri na tatizo la watoto watundu. 13. Mashaka- kutengwa kwa watoto walemavu kuanzia ngazi ya familia mpaka katika elimu. 14. Mtaji wa masikini- umuhimu wa utunzaji mazingira uanze kutolewa elimu ngazi ya shule.
Baadhi ya vitabu vyake vingine 1. Oldonyolenga 2. Utenzi wa mnazi 3. Bahati 4. Tusome kiushairi kitabu 1-2 5. Tuimbe Alfabeti 6. Mamba asili 7. Binti Afrika na rafiki kutoka China 8. Balozi Tunda-Safari ya bungeni 9. Sauti mafichoni 10. kisiwa cha kuzimu 11. Mwari wetu 12. Tungo za Rahma binti shaaban 13. Bustani ya kasri 14. Safari ya dubai 15. Safari ya Guangzhou China 16. Masikini chungu changu 17. Mizimu imekasirika
Filamu Kisiwa cha kuzimu- imeonyeshwa katika kituo cha televisheni ya taifa Tanzania (TBC) Mtunzi- Rahma Mahmoud Muongozaji mkuu- Rahma Mahmoud Muongozaji msaidizi- Masiha Muigizaji mkuu – Shamte kide (S. Kide)
Filamu zilizoigizwa bado hazijatoka 1. Filamu - Jambo usilolijua Mtunzi na muongozaji mkuu- Rahma Mahmoud Muigizaji mkuu - rashid Mtanga Maudhui - Malaria 2. Filamu- Safari ya ndege Mtunzi na Muongozaji mkuu- Rahma Mahmoud Maudhui- Ulemavu si pingamizi katika maisha
Filamu hizi zimetoka katika vitabu vyake na nyingine miswada.
Mashindano Rahma amekuwa akiandaa mashindano mbalimbali ya watoto juu ya uwandishi wa vitabu na kutoa zawadi. Aidha amekuwa akifundisha na kuhamasisha jamii hususani wanawake na watoto kuandika vitabu ili kuweza kupata nafasi ya kutoa mawazo yao, hasa ukizingatia ni moja ya jamii iliyopata misukosuko mingi ni wanawake na watoto. Harakati za Wanawake Rahma ameweza kuandaa na kuratibu warsha na semina mbalimbali juu ya uwandishi wa vitabu kwa wanawake Zanzibar, Kilimanjaro na pwani.
Warsha hizo zilipata ufadhili wa HIVOS.
Harakati za watoto
Amefanikiwa kufundisha watoto juu ya uandishi wa vitabu kati yao wawili alifanikiwa kuwachapisha vitabu.
Aidha amekuwa akiwafundisha watoto juu ya utangazaji na kutoa mawazo na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika siku ya utangazaji ya watoto akishirikiana times radio na unicef.
Aliungana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuwapeleka baraza la watoto bungeni mwaka 2005 ili kushinikiza bunge litambue haki zao na maombi yao ikiwemo ya kuruhusiwa kupata nafasi ya uwakilishi bungeni. Shughuli hii ilifadhiliwa na shirika la watoto duniani UNICEF.
Utafiti Katika kukuza fani yake ya uandishi wa vitabu alifanya utafiti wa mila na desturi za kumuandaa binti anayetoka katika utoto na kuwa mtu mzima(mwari) kwa makabila mbalimbali nchini Tanzania.
Tafiti hiyo ilijumuisha nyimbo zao, ndoa na historia fupi za wanawake katika harakati za kujiongezea kipato nchini Tanzania.
Mswada huo ulifanyiwa uhariri na mhadhari wa chuo kikuu cha Dar es salaam.
Ujasiriamali
Rahma mjasiriamali mdogo anayefanya biashara zake ndani na nje ya nchi akisafiri china na dubai.