Majadiliano ya mtumiaji:Moses

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Moses karibu kwenye wikipedia yetu! Naona umeanza kuchangia karibu tu! Nakuomba angalia mwanzoni makala ya msaada (unapata kiungo chake kwenye ukurasa wa Mwanzo). Itakusaidia kutafakari na kupanga vizuri makala zitakazolingana na masharti ya kamusi elezo. Labda anza na makala fupi - na uzoee namna ya kuandika katika Kamusi elezo pia jinsi gani kupanga na kuhariri makala. Ukipenda Ukiwa na swali uliza tu! --Kipala 13:17, 14 Februari 2007 (UTC)[reply]

Bwana Moses asante kwa jibu lako. Naona umependa hasa mambo ya dini. Inaonekana umesoma mengi una habari za kuchangia. Ila tu ningeshauri kweli ungeanza na mambo mafupi kwanza. Nikupe mfano: Makala ya Ubuddha umejitahidi lakini inafaa kugawiwa. Sehemu kubwa ya yaliyomo yake ni zaidi kuhusu Gautama Siddharta anayestahili makala yake pekee yake. "Buddha" ingekuwa makala nyingine kwa sababu katika Ubuddha wanajua mabuddha mbalimbali. Halafu "ubuddha" kama dini inahitaji habari zaidi hasa juu ya dini, historia yake, enezi, waumini, madhehebu.
Vivyi hivyo "Ukristo" ungepata vipengele vyake kulingana na masharti ya kamusi elezo. Ukipenda kuendelea maandishi yako naomba usikate tamaa ikibadilika sana siku moja. Naona pia ungetafakari kidogo juu ya tofauti kati ya hoja na habari za kihistoria. "Ukristo" kwa sasa hauonekani makala inataka kuelekea wapi. --Kipala 17:19, 15 Februari 2007 (UTC)[reply]