Majadiliano ya mtumiaji:Malangali
Malangali, kazi nzuri sana. Tupo pamoja! --Ndesanjo 26 Agosti 2006 (UTC)
Viungo
[hariri chanzo]Malangali, asante kwa orodha ya makabila! Kazi nzuri na msingi bora kwa wengine wanaoweza kuchangia!! Ni vizuri umekumbuka kuanzisha pia "Category". Nimeongeza sasa kiungo kwa "Jamii: Tanzania". Nimejifunza ya kwamba viungo hivi ni muhimu ili makala ipatikane kirahisi. Hata makala kadhaa za kwangu nilizoandika mwanzoni hazionekani tena nisipokumbuka jina kamili kwa sababu sikujali viungo na jamii.
Ukiendelea kutoa michango mema kumbuka na wewe jamii na viungo - kazi isiwe bure! --Kipala 13:41, 25 Agosti 2006 (UTC)
Majina
[hariri chanzo]Malangali, salamu sana. Umesahihisha majina ya nchi kadhaa katika makala ya "ikweta". Hapa hatuna makubaliano bado katika wikipedia hii. Kuna picha ya kwamba hakuna umoja bado kati ya wazungumzaji na waandishi wa Kiswahili jinsi gani kuandika majina ya nchi. Kuna namna nyingi za kutamka na kuandika. Kwa bahati mbaya kamusi kubwa (kwa mfano za TUKI) zimeacha majina haya kando. Wala hakuna namna moja katika vitabu vya Atlasi zetu nisipokosei.
Mara nyingi katika wikipedia tunafuata ama maandishi jinsi ilivyo katika nchi ile au karibu nayo; kama majina ya Kiswahili ya pekee yapo tunayatumia (Ufaransa, Uingereza); lakini wengine wanapendelea kama wewe kufuata sauti tu. Ila tu ukitaka kutumia maandishi kama "Ekwado" lazima uangalie mambo mawili: a) Je umbo hili linatumia au linakata marejeo kwa makala mengine - b) pili: Je maneno yanayofuata baada ya "Ekwado" katika mabano bado yana maana? Ningeona vema ukitaka kushughulika mambo haya chukua orodha yote ya Amerika Kusini tupate muundo moja. --Kipala 20:40, 22 Juni 2006 (UTC)
- Kipala, asante sana kwa kunikaribisha. Kuhusu majina ya nchi, kuna orodha nzuri inayopatikana kwenye Kamusi Hai. Orodha hii inafuata orodha tatu nyingine: zile za BAKITA, TUKI, na Redio Tanzania Dar es Salaam. Vikundi hivi vitatu vilisanifisha (au viliswahilisha, ukipendelea) majina ya nchi zote za dunia. Kama ulivyosema, mara nyingi hakuna makubaliano baina ya vyanzo mbalimbali, na orodha hiyo ya Kamusi Hai inaonyesha mitafaruku. Lakini kwa jumla orodha ya Kamusi Hai inaonyesha majina yaliyopendekezwa na wataalamu wa vyuo na waandishi wa habari. Je, tufuate mapendekezo haya, au tuhimize istilahi nyingine ya Kiwikipedia? Nafikiri ni afadhali tufuate njia moja na wao waliopewa cheti kusanifisha lugha rasmi, lakini naomba shauri lako.
- Orodha ya TUKI ilichapishwa katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la Pili, mwaka 2004, kurasa 473-477. Orodha hii ilifuata mapendekezo rasmi ya orodha ya BAKITA kutoka mwaka 2001, lakini ilibadili maneno mbalimbali (Ekwado badala ya Ikwado, kwa mfano). Baada ya hapo, Redio Tanzania Dar es Salaam ilipendekeza mabadiliko mengine mwaka 2005, kufuatana na matumizi yao. Mapendekezo yote yanaonekana katika orodha ya majina ya nchi iliyoandaliwa na Kamusi Hai ya Kiswahili kwenye Mtandao. Malangali 18:01, 23 Juni 2006 (UTC)
- Ndugu Malangali, nashukuru kwa jibu lako. Tunafurahia kila safari jina jipya lapatikana maana tuko wachache mno. Nasita kidogo kujibu namna gani. Kwanza nimefurahi kuona ordoha kwa sababu nimetafuta orodha ya aina hii na sijaikuta (nimewahi kutumia Kamusi Hai mara kadhaa ingawa kwa kusitasita kwa sababu nimeona kasoro mara nyingi; lakini inasaidia ukikaa kwenye kompyuta na kusikia uwivu kutembea tena hatua tano hadi rafu ya vitabu.Ila tu orodha hii sijawahi kukuta). Kwa bahati mbaya Kamusi yangu ya Kiswahili Sanifu ni toleo la kwanza hakuna orodha ya majina ya kijiografia.
- Kimsingi nakubali kabisa: tufuate ushauri wa wataalamu. Isipokuwa nikiona orodha hiyo ninasita. Mimi binafsi sipendezwi na mwelekeo wa „kupijinisha“ majina haya yote; yaani kuchukua majina ya asili katika lugha mbalimbali na kuyaandika kufuatana kwa matamshi ya Kiingereza kwa tahajia ya Kiswahili. (jinsi ilivyo kawaida katika lugha zinazoitwa „Pidgin english“ – hivyo kupijinisha). Nikiwa mpenzi wa etimolojia inaniudhi kusaga kila jina nzuri ya asili ya Kiarabu, Kilatini, Kigiriki, Kihindi n.k. kwa masikio ya Mwingereza kwanza na kufinyanga baadaye vumbi yake kwa ulimi wa Mswahili. Habari nyingi zinapotea kwa njia hii (kwa mfano ya kwamba jina la nchi ya Ecuador ni neno „ikweta“ tu kwa Kihispania – Ekwado inafaa kuwa chakula au kinywaji cha Kighana -TULE WAKISHINDA)
- Ninasita hasa kufuata orodha hii kwa kwa sababu tatu:
- siamini kweli ya kwamba wasomi wa Kiswahili kutoka Tanzania watakuwa msaada sana katika kujenga wikipedia. Maisha ya TZ ni magumu; msomi mwenye kutumia mitambo hii hatapenda sana kupoteza muda wake kuandika kwa wikipedia kazi isiyo na shukrani wala sifa kwenye chuo kikuu wala haina mapato (sijawahi kupata jibu baada ya jaribio la kuomba msaada kutoka watu mbalimbali huko). Sisi tulivyo ni ama Waswahili hasa wale walio mbali masomoni ya ng’ambo au watu wa nje waliojifunza na kupenda Kiswahili. Ningependa sana tuwe na maprofesa wawili watatu wa TUKI lakini hali halisi naogopa tutategemea kwa muda kidogo watu jinsi walivyo. Ila tujaribu kila namna kukaribisha wenyeji walioko TZ au EAK.
- Ninasita hasa kufuata orodha hii kwa kwa sababu tatu:
- nina wasiwasi ya kwamba orodha hii itafanya kazi na kusaidia. Wengi watakaotumia wikipedia kwa Kiswahili na kushirikiana kwetu ni watu waliopata elimu yao hasa kwa Kiingereza na lugha za nje; Wakenya kati yetu wanakosa hata masomo ya shule ya msingi kwa Kiswahili. Maana yake ni ya kwamba msamiati si pana sana; tukitumia umbo la kimaandishi ambalo ni mbali sana na yale waliyozoea tunaongeza ugumu wa kutumia wikipedia. Kodivaa, Babadosi au Aminya haisaidii bali kuleta ugumu. Sisomi hapa magazeti ya Tanzania: Je, wanafuata orodha hii au kwa kiasi tu? Kenya hawafuati – ni gazeti moja tu kwa Kiswahili.
- HASA sababu ya tatu ni: je,orodha hizi zinatosha kwa matumizi yetu? Nimetunga sasa sehemu kubwa ya makala ya nchi za Afrika (nadhani ziko kwenye orodha). Niko kwa miji mikuu (je, ziko zote katika orodha ya TUKI ???) pamoja na miji mingine na mito. Majina mengi wazee wa TUKI hawakuwahi kuangalia bado. Kama wikipedia hii inaendelea kupanuka jinsi ilivyo hata na watu wachache tunaendelea kilasiku kutaja majina yasiyopo kwenye orodha za TUKI n.k. Je tufanye nini? Kusubiri?
- Pendekezo langu: tusipoteze muda wetu kusahihishana (isipokuwa kama sahihisho la mtu mgeni inaharibu viungo kati ya makala) lakini tuendelee kushauriana. Kwa sasa tutumie mbinu za mtandao na hasa „mielekezo“: Ukipenda sana „Kodivaa“ lakini makala ya „Cote d’Ivoire“ iko tayari: andika makala fupi ya „REDIRECT“. Vilevile kama wewe umeandika makala ya „Ekwado“ mimi ningeweka REDIRECT nikitumia Ecuador. Mtandao na mitambo inatupa kiwango hiki cha uhuru.
- Unaonaje? --Kipala 20:48, 23 Juni 2006 (UTC)
Afrophonewikis
[hariri chanzo]Hujambo, Malangali. It took me some time, but I have finally become a member of the Afrophonewikis Group following your request to do so at my English talk page. Thanks for the heads up, I think the formation of this group is a step in the right direction. — mark ✎ 17:51, 26 Septemba 2006 (UTC)
Wabunge
[hariri chanzo]Malangali, hongera kwa makala za Wabunge na asante kwa kazi kubwa!! Je unaonaje kama ungeingiza pia chama na hasa jimbo la uchaguzi? Tovuti la bunge lina maelezo haya na ingeboresha wikipedia yetu kwa ujumla kwa sababu tunapata nafasi ya viungo. Mfano: Juma Jamaldin Akukweti ni Mbunge katika Bunge la Tanzania. Alichaguliwa katika jimbo la Tunduru ni mwanachama wa CCM.
Najua ni kazi hasa kwa sababu ya idadi kubwa ya makala lakini ukianza hivyo kwa wabunge utakaoweka? Pia nimeona tatizo la jamii "wanasiasa wa tanzania" iliyokuwa na REDIRECT kwa "wanasiasa Tanzania" hivyo wabunge hawakuonyeshwa. Nimetenganisha na kuwaweka zote mbili chini ya "watu wa Tanzania". Ukiwa na nafasi labda chungulia na kuhamisha wale wachache wa jamii "wanasiasa Tanzania" katika jamii uliotumia? --Kipala 20:44, 29 Novemba 2006 (UTC)
- Asante, Bw. Kipala. Kwa sasa, naona ni rahisi zaidi nikianzisha mbegu bila kuweka maarifa kama jimbo la uchaguzi. Ninachofanya naweza kufanya chapuchapu nikitumia mikasi na gundi. Baadaye itabidi kurudi kwenye kurasa za kila Mbunge na kuweka majimbo, siku za kuzaliwa, nk, lakini mwanzonimwanzoni napendelea kufanya bila kurudia kila mara kwenye dirisha jingine. Kama kuna mwengine anayetaka kufanya kama unavyopendekeza, lakini, karibu sana - wako zaidi ya Wabunge 300! :) Malangali 21:49, 1 Desemba 2006 (UTC)
Re: Vandalism
[hariri chanzo]Hi Malangali, please see this page for more information on page protection. And here's a link to view the current protection level for Mpira wa miguu. Link --Az1568 04:01, 12 Desemba 2006 (UTC)
- Since all your vandals on the page Mpira wa miguu are IP addresses, selecting "registered user only" will allow real users to make legitimate edits to the page but keep the IP spammers away. Also, check to see if the IPs are open proxies (en:open proxy). If they are, they may be indefinately blocked (m:WM:NOP).
- English WpA uses www.completewhois.com/rbl_lookup.htm to test for proxies. As an example, the first vandal to that page, User:69.74.139.149 is definately a proxy: www.completewhois.com/cgi-bin/rbl_lookup.cgi?query=69.74.139.149&display=webtable, likewise, so is User:80.75.0.253: www.completewhois.com/cgi2/rbl_lookup.cgi?query=80.75.0.253&display=webtable. Also check the IPs reputation on larger WMF wikis. For example User:83.143.18.69 has been blocked as an open proxy/zombie on the eN WpA: en:User talk:83.143.18.69. Similarly User:213.42.21.77 is definately block-worthy: www.completewhois.com/cgi2/rbl_lookup.cgi?query=213.42.21.77&display=webtable, User:81.21.176.10 is a Email and wiki SPAMmer: www.completewhois.com/cgi2/rbl_lookup.cgi?query=81.21.176.10&display=webtable , User:65.198.48.23 is evidently not a proxy, but has made repetitive robotic edits to other wikis. I'll try and remember to check back to this page, so you can ask questions here, or on my eN wikipedia talk page (en:User_talk:68.39.174.238). 68.39.174.238 03:53, 16 Desemba 2006 (UTC)
Mfumo radidia - tahajia
[hariri chanzo]Nd Malangali, nimeandika machache kuhusu chako kwenye makala hii. --Kipala 18:01, 13 Desemba 2007 (UTC)
Uchaguzi
[hariri chanzo]Kuna mapendekezo mapya kwa Wakabidhi na bureaucrat. Naomba angalia ukurasa http://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Wakabidhi --User_talk:Kipala 08:35, 1 Februari 2008 (UTC)
Changes at "MediaWiki:Common.css"
[hariri chanzo]We have a problem with the format of templates for info boxes. I consulted meta:user:Pathoschild who as a steward has given us advice before and he thought the reason was the deletion of "MediaWiki:Common.css" by you. I restored the file and the templates are fine. Probably you had some idea why you deleted this so kindly tell the community on "jumuiya". Pathoschild recommended also restoring MediaWiki:Monobook.js but I have no idea what that is for. Maybe its better to discuss such operations - this one left Muddy and me in the drak for some time. --User_talk:Kipala 18:40, 20 Februari 2008 (UTC)
- I was told to delete files that had been upgraded in the main version of MediaWiki, in order for the new version to be populated into sw.wikipedia. The issue was that new versions from Betawiki won't overwrite changes that have been made locally on individual projects, so system-wide changes weren't getting reflected on sw. If I remember correctly, the Common.css file had some comment along the lines of "deprecated in the new version". However, since that was the wrong thing to do, very sorry!
- In general, language localizations should always be done on Betawiki, so that the work is replicated on all sites that run MediaWiki. That wasn't the case in the old days, so I've been trying to get the projects in synch. Malangali 10:24, 25 Februari 2008 (UTC)
Vitufe vya kufanyia kazi
[hariri chanzo]Salam, Malangali. Nd. Kuna baadhi ya vifaa naona hamna katika wiki yetu. Na nimejaribu kuzungumza na Pathochlids kuhusu code za kuongezea vifaa hivyo (vitufe) akasema kwamba ni lazima ni mpate mtu aliye-mkabidhi ndiyo afanye kazi hiyo. Sasa unaweza ukapata kaji muda kadogo cha kufanya hiyo kazi? Basi ukiona umepata, naomba fungua hapa...--"Mwanaharakati" (talk) 06:08, 26 Februari 2008 (UTC)
Uteuzi mpya
[hariri chanzo]Kuna pendekezo jipya kwa bureaucrat. Naomba uangalie ukurasa wa wakabidhi. --Oliver Stegen 09:17, 1 Machi 2008 (UTC)
Mwanaharakati awe bureaucrat
[hariri chanzo]Nimemteua Mwanaharakati achaguliwe kuwa msimamizi mkuu pamoja nasi (b'crat). Naomba upige kura kwenye ukurasa wa wakabidhi. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 08:10, 28 Mei 2009 (UTC)
Flowerparty awe mkabidhi
[hariri chanzo]Nimemteua Flowerparty achaguliwe kuwa mkabidhi pamoja nasi. Naomba upige kura kwenye ukurasa wa Wakabidhi. Ahsante! --Mwanaharakati (Longa) 10:36, 9 Julai 2009 (UTC)
Flowerparty awe mkabidhi
[hariri chanzo]Nimemteua Flowerparty achaguliwe kuwa mkabidhi pamoja nasi. Naomba upige kura kwenye ukurasa wa Wakabidhi. Ahsante! --Mwanaharakati (Longa) 10:36, 9 Julai 2009 (UTC)
Kuondoa haki za usimamizi kwa baadhi ya watumiaji
[hariri chanzo]Malangali, salam! Unatakiwa utoe mawazo yako juu ya kuondoshwa kwa haki za usimamizi kwa baadhi ya watumiaji wasionekana kwa kipindi kirefu sana. Orodha hiyo unaweza kuipata hapa. Ahsante na kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 16:13, 10 Julai 2009 (UTC)
mradi wa Google kwa ajili ya wikipedia yetu
[hariri chanzo]Bwana Malangali, salaam!
Nimepata mawasiliano kutoka Christine Moon huko Palo Alto, California. Yeye anafanya kazi kwa shirika la Google, nao wameanza kupanga mradi au huduma kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania na Kenya ili waelimishwe kuandika makala kwa wikipedia ya Kiswahili. Kumbe!
Christine sasa ametualika kumwandikia maoni yetu, angalia tovuti hiyo:
http://docs.google.com/Doc?docid=0AbIPJ9Nv6udZZGd6MndwcGdfMzFkODNzOG0zYw&hl=en
Bahati mbaya yeye haelewi Kiswahili, kwa hiyo itakuwa lazima kumwandikia kwa Kiingereza. Asante kwa michango yako!
Ni wako katika ujenzi wa lugha yetu,
--Baba Tabita (majadiliano) 08:06, 10 Oktoba 2009 (UTC)
mkutano wa Skype kesho kutwa
[hariri chanzo]Ndugu Malangali, salaam! Jumatatu tarehe 19, saa kuminamoja za mchana/jioni (yaani saa za Nairobi) tutajaribu kukutana kwenye Skype kwa ajili ya majadiliano kuhusu kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Kenya na Tanzania kutumia na kuichangia makala wikipedia ya Kiswahili. Mpaka sasa tupo wanne: Christine wa Google (mooncheech), Sj (metasj), Muddyb (mohammed.lupinga) nami (stegling). Ni tumaini langu kuwa utakuwepo. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 18:57, 17 Oktoba 2009 (UTC)
majadiliano kuhusu utafsiri wa istilahi
[hariri chanzo]Bwana Malangali, salaam! Nimeanzisha majadiliano mapya kuhusu utafsiri wa istilahi ya wikipedia yetu hapa. Naomba uyaangalie na kuchangia maoni yako. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 09:37, 23 Oktoba 2009 (UTC)
Pendekezo kuhusu utaratibu wa kuanzisha makala kwa watumiaji waliojiandisha pekee
[hariri chanzo]naomba usome hapa na fanya uamuzi wako: Wikipedia:Jumuia#Pendekezo:_Utaratibu_wa_kuanzisha_makala Kipala (majadiliano) 14:59, 26 Novemba 2012 (UTC)
Karibu tena
[hariri chanzo]Salaam mMlangali - Karibu tena! Hujaonekana tangu muda mrefu. Uko salama? Nafurahi kukuona!! Kipala (majadiliano) 19:04, 19 Mei 2014 (UTC)
Kupakia mafaili, Sogora ya kupakia?
[hariri chanzo]Hello! Sorry for writing in English. As you're an administrator here, please check the message I left on MediaWiki talk:Licenses and the village pump. Thanks, Nemo 19:22, 18 Septemba 2014 (UTC)
Famouse Ukrainian People or maarufu Kiukreni
[hariri chanzo]- Hello Malangali! Sorry for writing in English. I don`t understand Swahili. I ask you to contribute with translation into the Swahili language. Could you or other users of your wikipedia translate some articles, that dedicated for prominent figures in Ukraine. The list shown on the page Wikipedia:Makala zilizoombwa. It is equipped interlanguage links and given pronunciation on Latin alphabet.--Yasnodark (majadiliano) 11:36, 10 Aprili 2016 (UTC)
Asking to a permission/advice/review
[hariri chanzo]Hi. I have a question. I would like to translate some articles to Swahili (mostly about computer science). But I don't speak Swahili. So, I've found the non-native Swahili speaker, making translations for money. But since I don't speak Swahili at all, I can't rate these translations by myself. The examples may be found on my page. Is the quality of the articles satisfactory? Should I place such articles to the public categories? Or should I place them in the sandbox or somewhere for review? Or the translations are just bad, and I search another translator? --DoctorXI (majadiliano) 00:53, 22 Desemba 2016 (UTC)
Tangazo
[hariri chanzo]Habari ndugu Mwanawikipedia!
Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA
Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo
Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.
Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia
Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.
Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 17:31, 5 Aprili 2020 (UTC)
Ukaguzi wa orodha ya wakabidhi
[hariri chanzo]Mpendwa, jina lako linapatikana kwenye orodha ya wakabidhi wa Wikipedia ya Kiswahili. Ilhali tutakagua orodha hiyo karibuni, nataka kukuuliza kama uko tayari kufanya kazi hii pia wakati ujao, pamoja na kushiriki katika shughuli za kuwa mkabidhi / admin. Naomba jibu lako ama kwa baruapepe kwangu au kwenye ukurasa https://sw.wikipedia.org/wiki/Majadiliano_ya_Wikipedia:Wakabidhi. Ndimi wako Kipala
Wakabidhi wenzangu,
tunahitaji kupeleka ukaguzi wa orodha ya wakabidhi tena mbele ya jumuiya. Kabla ya kuitagangaza hatua hii naomba tuelewane kwanza kati yetu kuhusu mambo mawili
1. Nani atapiga kura kati ya wanawikipedia? Pendekezo langu:
a) Mwenye kura awe aliyewahi kuandikishwa tangu mwezi 1 (hatutaki waliojiandikisha jana kwa kumpiga kura rafiki leo) b) aliyewahi kuhariri makala 3 kwenye swwiki (nje ya ukurasa wake mwenyewe; hatukubali watu walioingia kwa kutunga/kusahihisha makala 1 pekee) c) aliyehariri katika miezi 12 kabla ya kura yetu
Zamani tulikuwa wachache sana lakini siku hizi idadi ya waliojiandikisha imeongezeka ingawa wengi hawafanyi kitu tena, kwa hiyo tuelewane.
2. Kuhusu orodha ya wakabidhi kuna matatizo mawili: a) tunaendelea kutunza majina ya wengine ambao ama hawakushiriki kabisa tangu miaka, au hawakushiriki katika shughuli za usimamizi. (hapa nitamwandikia kila mmoja na kumwuliza kama yuko tayari kutekeleza shughuli za admin: kupitia mara kwa mara ukurasa wa Mabadiliko ya Karibuni, kuangalia makala mpya na mabadiliko, kufuta spam dhahiri, kupeleka makala zisizofaa kwenye ukurasa wa ufutaji, kushiriki katika ufutaji, kukaribisha wageni) LAKINI tunahitaji watu zaidi walio tayari kufanya kazi hii
b) tuelewane nipeleke swali namna gani:
ama tufute tu wale wasioshiriki tena na kuchagua wapya wa nyongeza (wale wanaofanya kazi waendelee tu) AU tufanye uchaguzi mpya kwa wote . Jambo hili si dhahiri na miradi ya wikipedia ziko tofauti hapa.
Naomba majibu kwenye ukurasa wa majadiliano ya wakabidhi. https://sw.wikipedia.org/wiki/Majadiliano_ya_Wikipedia:Wakabidhi
Ndimi wenu Kipala