Majadiliano ya mtumiaji:Lusajo Chicharito Brown

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Kipala (majadiliano) 18:07, 9 Aprili 2015 (UTC)[jibu]

Makala ya Black Leopard FC[hariri chanzo]

Nudu Lusajo, asante kwa michango. Kabla hujaendelea kuhariri naomba ujisomee kidoGo. Ujisomee Wikipedia:Mwongozo na hasa sehemu ya Wikipedia:Mwongozo_(Kumbuka)#Umuhimu:_Kuandika_juu_ya_nini.3F. Tatizo la hariri zako ni a) umetumia majina yasiyofaa kwa kamusi elezo, halafu unapenda kutangaza timu ya vijana ya klabu ndogo - je hii timu ina umuhimu gani ili iwe na makala hapa? Naomba ueleze umuhimu wake na uipange katika lugha inayolingana na kamusi elezo. Labda uangalie makala juu ya timu nyingine. (au ulize maswali maswali yako kwangu au kwa Mtumiaji:Muddyb_Blast_Producer) Kipala (majadiliano) 12:52, 11 Aprili 2015 (UTC)[jibu]

Ndugu Lusajo, naona umeongeza habari kuhusu Black Leopard FC. Sasa shida ni kwamba hatuna viungo kuonyesha umaarufu wa kilabu hicho. Nimeitafuta mtandaoni - hakuna! Naomba utusaidie kuonyesha umaarufu wa Black Leopard FC. Labda kuna insha gazetini au habari nyinginezo. La sivyo ingetubidi kufuta makala hiyo. Wasalaam, Baba Tabita (majadiliano) 07:17, 28 Aprili 2015 (UTC)[jibu]

Usiandike makala kuhusu mwenyewe[hariri chanzo]

Lusajo, si mzuri kuandika makala kuhusu mwenyewe. Ukiwa mashuhuri ya kutosha mtu mwingine ataandika makala kuhusu wewe. ChriKo (majadiliano) 23:07, 11 Aprili 2015 (UTC)[jibu]

Ukitaka kuweka ufafanuzi mfupi wa mwenyewe tafadhali uweke katika Mtumiaji:Lusajo Brown 'Chicharito'. Na kwanza angalia mifano, kama ukurasa wangu Mtumiaji:ChriKo na ule wa Kipala Mtumiaji:Kipala. ChriKo (majadiliano) 21:47, 14 Aprili 2015 (UTC)[jibu]


Muddy Kandonga[hariri chanzo]

Asante kwa mchano wako juu ya Muddy Kandonga. Naomba uiangalie upya. Je jina lake ni "Muddy" au "Mudy" ? Amezaliwa wapi ? Mwenyeji wa wapi? Amefanya nini kabla ya kuingia katika klabu? Naomba uongeze. Baadaye ni vema kama makala inaanza hivi: "Muddy Kandonge ni mchezaji wa kandanda wa Klabu ya.... . Amezaliwa tarehe ....... (mahali). Akasoma shule ya ......... Akajiunga na klabu (mwaka) .... halafu ...." Mwishoni usisahau kuipanga katika jamii husika. Pia agalia ukiandika usiache nafasi kwenye mwanzo wa mstari, tokeo haupendezi. Tazama ushauri hapo [[1]] na. 10. Wasalaam! Kipala (majadiliano) 07:52, 17 Mei 2015 (UTC)[jibu]

Asante kwa michango LAKINI usiendelee vile, wasiliana na kujifunza kwanza![hariri chanzo]

Sahihi: bofya hapa (katika dirisha ya hariri)

Salaam Lusajo asante kwa kuchangia. Kwa bahati mbaya kuna mambo kadhaa ambayo bado hujazoea. Naomba usiendelee kutunga vile lakini ujisomee kwanza wikipedia:Mwongozo. Unarudia kufanya makosa kadhaa. Nimekuandikia lakini hujajibu wala kuuliza maswali. Unaweza kunijibu muda wote ama hapa chini (bofya "Hariri chanzo" na andika chini matini yangu, halafu tia sahihi) au kwenye ukurasa wa majadiliano wangu Majadiliano_ya_mtumiaji:Kipala.

Makosa si magumu lakini makala haziwezi kukaa vile. Kama husahihishi kuna hatari ya kufutwa.

Kosa : unaanza mstari kwa nafasi tupu. Hii haitakiwa maana

inaleta picha vile

ambayo hatutaki.Soma hapa: Wikipedia:Mwongozo_(Anzisha_makala).

Kosa: usianze tena makala kwa maneno "Jina lake kamili ni". Nimeshakuandikia. Kama huelewi, basi uliza.

Kosa: Jitahidi kutumia tahajia sawa. Kwa lugha ya Kiswahili majina ya watu, nchi, miji huandikwa kwa herufi kubwa. Kwa hiyo si "Deus kaseke" bali "Deus Kaseke". Nimeisahisha lakini ni kosa baya inaweza kuharibu viungo vyote ndani ya wikipedia. Wasalaam Kipala (majadiliano) 10:52, 30 Mei 2015 (UTC)[jibu]

Bwana Lusajo, nimekuandikia mara kadhaa nikajaribu kukupa msaada jinsi gani kuchangia hapa. Naona sasa umetunga Oscar Fanuel Joshua kwa kurudia makosa yaleyale. Mpendwa kama unaona ugumu uliza maswali. Tuko tayari muda wote kuvumilia wageni na kuwsaidia. Hii nimekuambia mara kadhaa hujafanya wala hujajibu. Lakini kama hupendi kuheshimu utaratibu uliopo na kupuuza ushauri nitakuonya mara ujao halafu kukuzuia. Wasalaam. Kipala (majadiliano) 07:29, 17 Juni 2015 (UTC)[jibu]